Nahitaji Wakili Nifungue kesi dhidi Mkuu wa Wilaya na CCM-Nzega

afsa

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
1,986
Reaction score
1,585
Umefika wakati uvumilivu sasa basi! Tumeshuhudia/tumesikia Watumishi kujinyonga kwa maisha magumu(hasa walimu), Wananchi kujinyonga kwa maisha magumu, Wanafunzi kujinyonga kwa matokeo mabaya wala jamii ya watanzania haisituki hata kidogo. Sababu ya kufungua kesi dhidi ya MKUU WA WILAYA/CCM-NZEGA; 1. Kuzuia mkaa usipatikane zaidi ya miezi miwili sasa bila kuboresha/kurahisisha upatikanaji wa GESI au kupunguza bei ya UMEME badala yake umeme umepanda bei, mkaa wa kupikia umezuiwa 2. Bei za vyakula kuendelea kupanda huku mshahara ukibakia kuwa ule ule wenye makato chungu nzima 3. Kukosa ushirikiano wa viongozi pale linapotokea tatizo linalohitaji msaada wa viongozi kama MKUU WA WILAYA, MKURUGENZI, OCD, MKUU WA IDARA . Haya ndo mambo yamenifanya nimtafute WAKILI ili anisaidie kufungua kesi dhidi ya CCM/MKUU WA WILAYA Kubwa HASA ni KUJINYONGA kwa wananchi kunakosababishwa na MAISHA MAGUMU KABLA "SIJAJINYOGA" . Nakumbuka MISRI vuguvugu la mapinduzi lilipamba moto baada ya kijana mmoja kujitia moto.TWENDE MAHAKAMANI
 
mkuu ungefungua kesi dhidi ya jk aliyetuahidi maisha bora kwa kila mtz na hatujayaona
 
mkuu ungefungua kesi dhidi ya jk aliyetuahidi maisha bora kwa kila mtz na hatujayaona

Nataka nianze na saizi yangu MKUU WA WILAYA
 
Nataka nianze na saizi yangu MKUU WA WILAYA

Huyo mama tumewahi mbana sn wakati wa sensa Bukene huko.Walikuwa wanatuchezea pesa za seminar,mbona alikaa
 
Huyo mama tumewahi mbana sn wakati wa sensa Bukene huko.Walikuwa wanatuchezea pesa za seminar,mbona alikaa

Naanza nae huyu maana maamzi yake hayana tija kwa wananzega mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…