afsa
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 1,986
- 1,585
Umefika wakati uvumilivu sasa basi! Tumeshuhudia/tumesikia Watumishi kujinyonga kwa maisha magumu(hasa walimu), Wananchi kujinyonga kwa maisha magumu, Wanafunzi kujinyonga kwa matokeo mabaya wala jamii ya watanzania haisituki hata kidogo. Sababu ya kufungua kesi dhidi ya MKUU WA WILAYA/CCM-NZEGA; 1. Kuzuia mkaa usipatikane zaidi ya miezi miwili sasa bila kuboresha/kurahisisha upatikanaji wa GESI au kupunguza bei ya UMEME badala yake umeme umepanda bei, mkaa wa kupikia umezuiwa 2. Bei za vyakula kuendelea kupanda huku mshahara ukibakia kuwa ule ule wenye makato chungu nzima 3. Kukosa ushirikiano wa viongozi pale linapotokea tatizo linalohitaji msaada wa viongozi kama MKUU WA WILAYA, MKURUGENZI, OCD, MKUU WA IDARA . Haya ndo mambo yamenifanya nimtafute WAKILI ili anisaidie kufungua kesi dhidi ya CCM/MKUU WA WILAYA Kubwa HASA ni KUJINYONGA kwa wananchi kunakosababishwa na MAISHA MAGUMU KABLA "SIJAJINYOGA" . Nakumbuka MISRI vuguvugu la mapinduzi lilipamba moto baada ya kijana mmoja kujitia moto.TWENDE MAHAKAMANI