Gharama za drip irrigation hutegemea na mambo mbali mbali kama
1.Aina ya zao unalotaka kumwagilia
Mfano dripline za papai ni tofauti na zile za nyanya, hoho na mazao mengine ya mboga mboga kwa hyo Gharama pia hutofautiana
2. Shamba lilivyokaa (topography) na mapendekezo ya mteja
Drip irrigation kwenye shamba ambalo ni flat hutofautiana na shamba ambalo lina mwinuko au mteremko kwa sababu shamba la namna hii utahitaji kuligawa katika plot (head units) ndogo ndogo ili utokaji wa maji uwe sawa kwa kila mmea tofauti na shamba ambalo ni flat lisilo hitaji kugawanywa
Pia mteja anaweza kuamua kugawa shamba lake kwenye plots mfano wateja wengine wanaweza kuamua hekari moja igawanywe mara mbili na kila nusu hekari anaotesha zao tofaut so gharama hapa zitatofautiana
3. Materials zinazotumika
Katika drip irrigation zipo materials kutoka kampuni mbalimbali zenye specifications na ubora tofaut mfano tuongee issue ya wall thickness. Zipo drip zenye wall thickness ya 1mm, 0.6mm, 0.4mm(hizi ndio nyingi sokoni)., 0.2mm na pia zipo dripline za round, flat na nyingine ni pressure compensation na pia zipo za self flushing so Gharama pia zinategemea unatumia materials gani na kutoka kampuni gani mfano Netafim, captain, azud, toro, john Deere, irritec, green agriculture, sertan, vishaka, mertplus, irrist, approtech na nyingine nyingi
Kwa kumalizia kama mkulima unahitaji irrigation system angalia zaidi ubora wa kati na uchukue material ambazo unaweza kuzitumia angalau kwa miaka mitano ili uweze kurudisha Gharama Zako
Pia tafuta mfungaji mzuri ili system yako iweze kufanya kazi kwa tija nzuri
Pia hakikisha unawekeza pia kwenye usimamizi wa mradi wako ili uweze kupata faida kwani unaweza kuwekeza sana kwenye infrastructure na kusahau kuwa usimamizi na agronomia ni msingi. Mfano ukikosea kupiga dawa au kuweka mbolea utaishia kupata hasara na kulaumu drip irrigation [emoji3]
Kwa maelekezo haya karibu tukuhudimie sisi tunafanya design, installation pamoja na uuzaji wa vifaa vya irrigation tupo morogoro mjini na dsm mikocheni
0763347985 / 0673000103
Gharama zetu ni 2.5mil-3mil kulingana na factor nilizoeleza hapo juu
Sent using
Jamii Forums mobile app