Prof.Mbwete, Prof Masenge,+++++++++++ ni waalimu wa sekondari kweli? Big no. of (90) wahadhiri wa OUT ni kutoka UDSM, wasaidizi ni wale waliokuwa Tutorial Asst hapo UDSM na baadhi ya wastaafu wa hapo mlimani.
Narudia tena, aina ya usomaji wa OUT hauwezi kufanana na UDSM kwa sababu nyingi sana, aina ya udahiri wa wanafunzi, mfumo wa digrii zao lakini pia wanafanana sana na Cambridge Inter. College ktk ku groom students wao.
nakupa mfano sasa CIC wanatoa Bachela ktk menejiment/Uchumi/masoko kwa two years lakini wanazingatia nini ktk hilo, ni lazima mfano mtu wa marketing- atatakiwa awe CIC diploma1- Sales Management & Marketing, 2.Global Marketing 3.Advertising &Public Relation, sasa wanakutaka walau uwe umehitimu hizi diploma mbili ili wao waweze ku discount baadhi ya topics ktk degree program yako. Kwa ufupi CIC Degree inapatikana kwa kuzingatia Education and Carrier historical back ground yako, wanachokuongezea ni vile unavyovikosa na automatically umeitia mkononi degree yako. Kwa jinsi wabongo tulivyo wapenda maneno utaona watu wanahoji why 2yrs? wanasahau kuwa hizo diploma hukuziokota msalani na kwamba study, mitihani,mazoezi na time ilitumika mpaka CIC wakakubali kuwa 2yrs is enough for a student.
Out wanaelekea huko na ndiko dunia iliyosonga mbele waliko ila kwa vile mazoea hujenga tabia basi tutang'ang'ania tulipo tu.
KUMBUKENI MUNGAI ALIPOSEMA 2YRS YA DIPLOMA YA ELIMU KWA WALIMU WA SEKONDARI NI SAWA NA MWANAFUNZI ALIYEMALIZA 1ST YEAR YA UNIVERSITY, HIVYO AKIJUNGA NA UNIVERSITY BAADALA YA 3YRS NI TWO YRS , LOOOH IKALETA MANENO SANA NA SIDHANI KAMA IMEANZA KUWA IMPLEMENTED AU LA, IDEA HIYO YA MZEE MUNGAI ILIENDA SAMBAMBA NA KUVIPA NGUVU VYUO VYA KLERUU,MARANGU,KIGURUNYEMBE NA KILE CHA MTWARA KUZALISHA KADA HIYO YA WALIMU BAADALA YA MKWAWA NA CHANG'OMBE AMBAO SASA WANATOA DIGREE YA ELIMU. TANZANIA TUBADILIKE WAKUU, TUSIPONDE KILA FURSA BALI TUZIIMARISHE NA TUHESHIMU MCHANGO WA WALE WANAOJITOLEA KULETA MABADILIKO HAYO MAANA WANADUMU KTK HISTORIA YA NCHI YETU KWA VIZAZI NA VIZAZI.