Nahtaji serious business partners wa ufugaji wa kuku wa mayai

Asbm

Member
Joined
Jun 26, 2019
Posts
38
Reaction score
33
Ndugu zanguni,heri ya mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Kama maada hapo juu inavojieleza. Nahtaji serious partners kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa mayai kibiashara.Mahali pa ufugaji ni mkoani Iringa ambapo ndipo mabanda yalipo yenye uwezo wa kufuga kuku zaidi ya elfu 10 wa mayai.

Partner anayetaka kujiunga ni awe na uwezo wa kufuga kuku 1,000.Gharama kwa kuku hao ni m 15 hadi wanaanza kutaga(baada ya week 20 au miezi 5).Hizo ni ghrama kwa ajili ya vifaranga,chakula,chanjo na madawa.

Mategemeo ni kuwa

Asilimia 80% ya kuku watataga,hivo kila kuku 1,000 wa mayai,kuku 800 watataga kwa siku hivo kupata tray 26 kwa siku. Ukizidisha na Tsh.5,000 kwa tray itapatikana Tsh.150,000 kwa siku.Hapo wakianza kutaga kutakuwa na gharama za chakula ili waendelee kutaga zaidi

Kwa aliye serious anaweza ni pm

Ahsante
 
Standard ya gharama za kulisha kuku mmoja wa mayai hadi kutaga ni Tsh 16,000/

Kwa kuku 1000 kuwalisha tu ni 15 Milion hadi 16. Hapo ni msosi pekee yake, Vifaranga 1000 ni Tsh2,500,000/ hapo bado vitu kama Nishati ya kuwakuza wakiwa wadogo, Vyombo vya kulia na kunywea hujasema kama unavyo, Gharama za kusafirisha Chakula hadi shambani. Bado madawa na Chanjo.

Kwa kifuli kuku 1000 uwe na milion 20+

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napenda hesabu za kilimo na ufugaji[emoji4]!simpo mathematics[emoji28]
Hahahahah, Mimi ongezea Ma Inspirational speakers., Wale nilianza mgahawa kwa mtaji wa 5000, now Nina migahawa miwili Posta na Masaki na nataka kufungua mwingine Nairobi..., Very funny [emoji23][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru kwa maelezo mazuri mkuu.Kiukweli upo sahihi sana.Kuhusu vyombo vya kufugia na gharama za kusafirishia chakula vipo ila pia itakuwa na makubaliano kati ya partners
 
Mchanganuo bado haujashiba especially kwenye kitu muhimu sana kwa mwekezaji ambacho ni soko LA hyo mayai lilipo na faida kwa ujumla

Sent using Jamii Forums mobile app
Soko ni kubwa sana mkuu.Nashukuru kwa mchango wako.Cjafanikiwa tu kuattach doc inayoonyesha demand ya mayai kwa Dar pekee yake.Nitafanya hivo
 
Mbona inawezekana na tunawaona watu wa mafanikio hayo, ila huwa ni miaka mingi sanaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kujaribu ni bora kuliko kukaa kimya
 
hua nacheka sana kwenye seminar zao yaan wana rahisisha mambo utadhani maisha ni simple ki hivyo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una uzoefu wa miaka mingap kwenye huo ufugaji? Je, ulishawah kuwa na partnership na mtu kwny hiyo issue?
 
Una uzoefu wa miaka mingap kwenye huo ufugaji? Je, ulishawah kuwa na partnership na mtu kwny hiyo issue?
Nina uzoefu usiopungua miaka 3 mkuu.Cjawahi kuwa na partners before
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…