JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Takwimu hizo zinaonesha kuwa kuna upungufu wa makosa 164 sawa na Asilimia 12.8 yakiwemo Makosa ya Kubaka na Kulawiti.
Akitoa tathmini ya hali ya usalama Zanzibar kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2024 huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar CHEMBERA ameeleza kuwa katika kipindi cha Januari hadi Disemba, 2024, jumla ya makosa 829 ya kubaka yameripotiwa ikilinganishwa na makosa 927 ya kipindi kama hicho Mwaka 2023 ni upungufu wa mako sa 98 sawa na Asilimia 10.6.
Aidha, amesema kuwa katika kipindi cha Januari hadi Disemba, 2024 jumla ya makosa 217 ya kulawiti yameripotiwa ikilinganishwa na makosa 309 ya kipindi kama hicho Mwaka, 2023, ni upungufu wa makosa 92 sawa na Asilimia 29.8.
Makosa yaliyochambuliwa katika kundi hili ni Uvunjaji, Wizi wa Mifugo.
UVUNJAJI
Katika kipindi cha Januari– Disemba 2024,Jumla ya makosa 823 ya uvunjaji yameripotiwa ikilinganishwa na makosa 833 ya kipindi kama hicho mwaka, 2023. Ni Upungufu wa makosa 10 sawa na asilimia 1.2 . Vyanzo vya makosa haya, Kuwania mali/kipato na ushawishi wa makundi.
Katika kipindi cha Januari – Disemba, 2024,Jumla ya makosa 370 ya wizi wa mifugo yaliripotiwa ikilinganishwa na makosa 244 ya kipindi kama hicho mwaka, 2023. Hili ni ongezeko lamakosa 126 sawa na asilimia 51.6.
MAKOSA DHIDI YA MAADILI YA JAMII
Jumla ya matukio 174 ya maadili ya jamii yameripotiwa katika kipindi cha Januari – Disemba, 2024 ikilinganishwa na matukio 176 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka,2023. Ni upungufu wa matukio 02 sawa na asilimia 1.1. Makosa yaliyochambuliwa kwenye kundi hili ni Heroine, Bhnagi, Mophem na Pombe moshi.
MATUKIO DHIDI YA WAGENI (WATALII)
Kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Disemba, 2024, jumla ya matukio 302 dhidi ya Watalii yameripotiwa ikilinganishwa na matukio 181 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho cha mwaka,2023. Ni ongezeko wa matukio 121 sawa na asilimia 66.8.
MAKOSA YA USALAMA BARABARANI
Katika kipindi cha Januari – Disemba, 2024, makosa 49,789 yameripotiwaikilinganishwa na makosa 38,895 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka, 2023. Ni ongezeko la makosa 10,894 sawa na asilimia 28.0.
Vyanzo vya matukio haya ni, sababu za kibinadamu ikiwemo mwendokasi, Uzembe wa madereva, ulevi na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.