JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Akitoa tathmini ya hali ya usalama Zanzibar kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2024 huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar CHEMBERA ameeleza kuwa katika kipindi cha Januari hadi Disemba, 2024, Jumla ya makosa 66 yameripotiwa ikilinganishwa na makosa 44 ya Mwaka 2023.
Amesema hiyo ni ongezeko la makosa 22 sawa na Asilimia 50, ambapo amesema makosa mengi ya mauaji yametokana na baadhi ya Wananchi kujichukulia Sheria mikononi.
Amewataka Makamanda wa Polisi wa Mikoa pamoja na Maafisa wa Polisi kuongeza nguvu katika kuzuwia makosa ya Mauaji, wizi wa pikipiki, Wizi wa mifugo, makosa dhidi ya watalii na makosa ya usalama barabarani ambayo yameongezeka mwaka 2024 ikilinganishwa na mwaka 2023.
Aidha, amewahimiza kushirikiana na jamii, vikosi vya ulinzi na usalama na taasisi za haki Jinai katika utekelezaji wa majukumu yao.