City Of Lies
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 4,925
- 6,137
Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu amekamatwa katika mahakama ya juu zaidi Nairobi kutokana na tuhuma za rushwa.
Jaji Mwilu amepelekwa katika makao ya idara ya uchunguzi wa uhalifu DCI kuhojiwa.
Ni kiongozi wa juu serikalini kukamatwa katika operesheni ya serikali kukabiliana na rushwa nchini.
Muda mfupi baada ya kukamatwa, mwendesha mashtaka mkuu nchini Noordin Haji ameitisha mkutano wa dharura na waandishi wa habari kuhusu suala hilo.
BBC Swahili