View attachment 857460
Naibu Jaji Mkuu nchini Kenya, Philomena Mwilu ametiwa nguvuni wiki iliyopita nchini Kenya na kukabiliwa na mashitaka 13, yakiwemo: usimamizi mbaya wa mamlaka; kukosa kulipa kodi na kujipatia Ksh. milioni 12 kwa njia ya udanganyifu kutoka Benki ya Imperial iliyoanguka kufuatia misukomisuko ya usimamizi mbaya. Kiongozi wa Mashitaka ya Umma, Noordin Haji, alisema kuwa, Mwilu anafaa kuhukumiwa na kufungwa kwa uhalifu.
Mawakili wapatao 32 walikuwa wamejitayarisha vilivyo kumwakilisha wakiongozwa na Seneta wa Siaya, James Orengo na Kiongozi wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka.
Hata hivyo, Mwilu anamtuhumu Kenyatta kwa kutaka kumuondoa katika Idara ya Mahakama. Anasema kumekuwa na majaribio mbalimbali ya kumlazimisha aache kazi yake kufuatia uamuzi wa matokeo ya Uchaguzi ya urais ambayo yalifutiliwa mbali na kulazimu Uchaguzi mwingine Oktoba 26, 2017. Hata hivyo, Rais Kenyatta amemjibu Mwilu na kumwambia abebe msalaba wake na aache kumhusisha na shida zake.
Mchambuzi wa masuala ya Siasa nchini humo, Mutahi Ngunyi, amemuonya Jaji Mkuu David Maraga akae chonjo baada ya masahibu kumkumba Naibu wake.
Aidha, wachambuzi wa Siasa wanadai mashitaka hayo ni mbinu ya Jubilee kumuondoa Mwilu ili asimrithi Jaji Maraga atakapostaafu mwaka 2022, ambao ni mwaka wa uchaguzi. Inadaiwa Jubilee wanataka Jaji Njoki Ndunguru ndiye arithi nafasi hiyo kwa kuwa, alikuwa mmoja wa majaji watatu waliopinga uamuzi wa kutupilia mbali matokeo ya urais mwaka jana. Philemona Mwilu ndiye alibebeshwa jukumu la kusoma uamuzi wa Mahakama wa kutengua matokeo ya Uchaguzi wa awali uliompa Uhuru ushindi.
Baada ya Mahakama kutengua matokeo ya awali, Uhuru alighadhabika na kutoa onyo kali kwamba,
majaji waliomwaibisha wangeona kilichomtoa kanga manyoya. Aliwaita majaji hao wanne
wakora na
kuapa kuwafunza adabu.
Vilevile, Septemba 2, 2017, Uhuru alihoji
"Nani aliwachagua? Mlichaguliwa? Tuna shida na kwa hakika turaitatua."
View attachment 857458
CHADEMA yatangaza kumuunga mkono Rais Kenyatta katika uchaguzi ujao wa Kenya
MBOWE,LOWASSA WAMPONGEZA KENYATTA KUCHAGULIWA TENA KUONGOZA KENYA - MALUNDE 1 BLOG
View attachment 857461
Baba wa Demokrasia Afrika Mashariki!!!
View attachment 857462
CHADEMA chini ya Lowassa wakimnadi Uhuru Kenyatta umasaini.