Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu akamatwa kwa tuhuma za rushwa

Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu akamatwa kwa tuhuma za rushwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu amekamatwa katika mahakama ya juu zaidi Nairobi kutokana na tuhuma za rushwa.

Jaji Mwilu amepelekwa katika makao ya idara ya uchunguzi wa uhalifu DCI kuhojiwa.

Muda mfupi baada ya kukamatwa, mwendesha mashtaka mkuu nchini Noordin Haji ameitisha mkutano wa dharura na waandishi wa habari kuhusu suala hilo

1.jpg

=======

Deputy Chief Justice Philomena Mwilu has been arrested at Supreme Court in Nairobi over alleged corruption.

Judge Mwilu was on Tuesday taken to the Directorate of Criminal Investigations for questioning.

Moments after the arrest, Director of Public Prosecutions Noordin Haji called an urgent press conference on the matter.

Her arrest followed a series of meetings by the Judicial Service Commission, the judiciary employer, for the better part of the morning.

Interestingly, Judge Mwilu also attended the meetings and it is not clear if she was being grilled by her employer.
 
IMG_7775.JPG


Naibu Jaji Mkuu nchini Kenya, Philomena Mwilu ametiwa nguvuni wiki iliyopita nchini Kenya na kukabiliwa na mashitaka 13, yakiwemo: usimamizi mbaya wa mamlaka; kukosa kulipa kodi na kujipatia Ksh. milioni 12 kwa njia ya udanganyifu kutoka Benki ya Imperial iliyoanguka kufuatia misukomisuko ya usimamizi mbaya. Kiongozi wa Mashitaka ya Umma, Noordin Haji, alisema kuwa, Mwilu anafaa kuhukumiwa na kufungwa kwa uhalifu.
Mawakili wapatao 32 walikuwa wamejitayarisha vilivyo kumwakilisha wakiongozwa na Seneta wa Siaya, James Orengo na Kiongozi wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka.
Hata hivyo, Mwilu anamtuhumu Kenyatta kwa kutaka kumuondoa katika Idara ya Mahakama. Anasema kumekuwa na majaribio mbalimbali ya kumlazimisha aache kazi yake kufuatia uamuzi wa matokeo ya Uchaguzi ya urais ambayo yalifutiliwa mbali na kulazimu Uchaguzi mwingine Oktoba 26, 2017. Hata hivyo, Rais Kenyatta amemjibu Mwilu na kumwambia abebe msalaba wake na aache kumhusisha na shida zake.
Mchambuzi wa masuala ya Siasa nchini humo, Mutahi Ngunyi, amemuonya Jaji Mkuu David Maraga akae chonjo baada ya masahibu kumkumba Naibu wake.

Aidha, wachambuzi wa Siasa wanadai mashitaka hayo ni mbinu ya Jubilee kumuondoa Mwilu ili asimrithi Jaji Maraga atakapostaafu mwaka 2022, ambao ni mwaka wa uchaguzi. Inadaiwa Jubilee wanataka Jaji Njoki Ndunguru ndiye arithi nafasi hiyo kwa kuwa, alikuwa mmoja wa majaji watatu waliopinga uamuzi wa kutupilia mbali matokeo ya urais mwaka jana. Philemona Mwilu ndiye alibebeshwa jukumu la kusoma uamuzi wa Mahakama wa kutengua matokeo ya Uchaguzi wa awali uliompa Uhuru ushindi.

Baada ya Mahakama kutengua matokeo ya awali, Uhuru alighadhabika na kutoa onyo kali kwamba, majaji waliomwaibisha wangeona kilichomtoa kanga manyoya. Aliwaita majaji hao wanne wakora na kuapa kuwafunza adabu.
Vilevile, Septemba 2, 2017, Uhuru alihoji "Nani aliwachagua? Mlichaguliwa? Tuna shida na kwa hakika turaitatua."

IMG_7774.JPG

CHADEMA yatangaza kumuunga mkono Rais Kenyatta katika uchaguzi ujao wa Kenya

MBOWE,LOWASSA WAMPONGEZA KENYATTA KUCHAGULIWA TENA KUONGOZA KENYA - MALUNDE 1 BLOG

IMG_7777.JPG

Baba wa Demokrasia Afrika Mashariki!!!


IMG_7779.JPG

CHADEMA chini ya Lowassa wakimnadi Uhuru Kenyatta umasaini.
 
Back
Top Bottom