GE2025 Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana CCM, Mussa Mwakitinya, asisitiza Mshikamano baada ya vikao vya uteuzi, Tabora

GE2025 Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana CCM, Mussa Mwakitinya, asisitiza Mshikamano baada ya vikao vya uteuzi, Tabora

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Mussa Mwakitinya (MNEC) amewasihi viongozi wana CCM mkoa wa Tabora, kuendelea kuwa wamoja na kuzuia mipasuko inayoweza kukipata Chama wakati mgumu wa kuitafuta Dola

Mwakitinya ameyasema hayo mara baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM cha Mkoa wa Tabora ambacho kilifanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea udiwani watakaopeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba mwaka huu

“Tunaamini mchakato huu utatuacha tukiwa wamoja na wenye mshikamano kwa misingi ya kwamba tuna kazi kubwa zaidi mbele yetu ya kuendelea kutafuta Dola, tukiendelea kumeguka vipandevipande inaweza kuwa ni changamoto kwetu”

Mwakitinya pia alisitiza suala la utunzaji wa siri mara baada ya vikao, kwani utunzaji wa siri ni sifa mojawapo ya viongozi wa CCM.

"Jambo kubwa tuendelee kutunza siri, moja ya sifa ya kiongozi ni utunzaji wa siri, kama kiongozi ukienda kutoa siri ambayo hatujakubaliana kwenye kikao, hii maana yake moja kwa moja safari yako ya kisiasa utakua umeihitimisha mara baada ya kumaliza kikao hicho"




Chanzo: UVCCM Tz
 
Back
Top Bottom