Pre GE2025 Naibu katibu UVCCM Taifa, Mwatikinya: Ushindi kwa CCM sio ombi ni lazima. Hakuna Chama kinaweza tatua shida za Wananchi zaidi ya CCM

Pre GE2025 Naibu katibu UVCCM Taifa, Mwatikinya: Ushindi kwa CCM sio ombi ni lazima. Hakuna Chama kinaweza tatua shida za Wananchi zaidi ya CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Naibu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Taifa bara, Mussa Mwatikinya amesema ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotegemewa kufanyika mwaka huu ni lazima na wala sio ombi.

Akizungumza leo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro katika uzinduzi wa kambi la Vijana wa jumuiya wa jumuiya hiyo, Mwatikinya amesema hakipo chama ambacho kinaweza kuongoza nchi na kuwaletea wananchi maendeleo zaidi ya CCM.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha amesema katiba ya chama hicho inadema lengo kuu la kwanza la CCM ni kushika dola, kwa kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro Ivan Moshi amesema mitano tena ni kwa Rais pekee hivyo vijana wajitokeze kugombea nafasi za ubunge na udiwani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM Moshi Vijijini Yuvenal Shirima amesema kambi hiyo ya vijana itakua ni chachu ya kuwajenga na kuongeza ari na utii kuelekea katika uchaguzi mkuu.

 
Yupo sahihi,Wala sio mwaka huu tu,CCM imekuwa ikilazimisha matokeo kwa mtutu wa bunduki kwa miaka mingi tu,ila mwaka huu hakuna uchaguzi.
Wajiandae na reforms
 
Back
Top Bottom