Naibu Msajili Mahakama ya Uhujumu aainisha masharti ya kusikiliza kesi ya Mbowe

Wadau wa kimataifa wanazidi kuweka mbinyo kuwa haki siyo itendeke bali pia ionekane inatendeka katika mwenendo mzima wa kesi hii siku hadi siku ikiwamo hukumu itakayotolewa .
 
..kwanini mshitakiwa mmoja amefungwa pingu huku wenzake wakiwa hawana?

Cc Petro E. Mselewa , Pascal Mayalla, Erythrocyte
Yule anayefungwa pingu ni komandoo wa jeshi la wananchi , wanahofu uwezo wake wa kupiga unaweza ukaleta shida , ndio maana anafungwa pingu .

Nimeona swali lako kitambo ila device niliyokuwa natumia ilihujumiwa sikuweza kujibu , sasa nina device mpya
 
16 SEPTEMBER 2021
Mahakama Kuu
Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhumjumu Uchumi

Wakili msomi Emmanuel Agostino anatoa muhtasari-fafanuzi wa yaliyojiri Leo

Kesi ya Mbowe siku ya pili Alhamisi tarehe 16 September 2021 inasimuliwa na wakili ambaye alikuwepo mahakamani.

Source: channel1TV

Je Media kubwa za Televisheni / Radio Stesheni Tanzania zimeshindwa kupata mojawapo ya nafasi za waandishi kuwepo mahakamani?
 
Yule anayefungwa pingu ni komandoo wa jeshi la wananchi , wanahofu uwezo wake wa kupiga unaweza ukaleta shida , ndio maana anafungwa pingu .

Nimeona swali lako kitambo ila device niliyokuwa natumia ilihujumiwa sikuweza kujibu , sasa nina device mpya

..hao wengine wawili sio makomandoo?

..na mwenye pingu ndio mshtakiwa wa kwanza?

..kwanini Mbowe sio mshtakiwa wa kwanza wakati yeye ndiye anatuhumiwa kuwa chanzo cha mpango mzima, na mfadhili mkuu?

..hii kesi imekaa kiajabu-ajabu.

Cc Petro E. Mselewa
 
Kwanini mahakama isihamie uwanja wa Mkapa ili wananchi wengi tupate nafasi ya kufika na kusikiliza na kujionea kwa macho kila kitu na tushudie sheitwani akiangukia pua[emoji2][emoji2]
Ufinyu wa nafasi mahakamani unaondoa haki ya wanaotaka kusikiliza kesi?
 
Bila kurekodi waandishi wa habari watakuwa wamekwazwa.
 
Hii kesi ya kihistoria inatafutia kila namna kumbukumbu zake zisiwepo mitandaoni on real time.

Wanataka tuishie kuona waandishi wa mitandaoni kutuonesha jinsi gari la karandiga lilivyoingia kwa madoido Mahakamani kisha kuondoka kwa kasi ndiyo iwe habari ya kilichojiri mahakamani kila siku!
 

Afisa kipenyo huyo. Sarakasi juu ya sarakasi.

Ule mhimili uliojichimbia ni mwendo wa kutoka kivingine.

Waweke live kwenye TV ili nafasi za kuhudhuria mahakamani zitoshe. Hii itaondoa kelele na simu.

Bila ya kupambania Katiba mpya kwa nguvu na ari zaidi, safari bado sana.
 
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu anasema hawakufurahishwa namna mwenendo mzima wa kesi ulivyoripotiwa na kurushwa mitandaoni kupitia simu za watu waliokuwapo Mahakamani
Kwani wasipofurahishwa kuna sheria yoyote ya kufurahishwa inakuwa imevunjwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…