Naibu Spika, Zungu: Marufuku kuvaa sare za Chama bungeni

Naibu Spika, Zungu: Marufuku kuvaa sare za Chama bungeni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katika kusimamia mavazi rasmi ya wabunge, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge imebaini kuwa baadhi ya wanaoingia maeneo ya Bunge huvaa sare zinazoashiria au kuzoeleka kuvaliwa na wafuasi au mashabiki wa vyama vya siasa kwa alama, nembo, maandishi ambavyo hutafsiriwa kwa jina, alama, msemo au nembo ya chama.

Kamati hiyo imependekeza kuweka kanuni inayokataza mavazi hayo ili kudumisha dhana ya Bunge kuendesha shughuli zake kwa uhuru na umoja bila kujali itikadi za kisiasa.

Aidha, kanuni kuhusu mavazi imeboreshwa ili kuweka usimamizi madhubuti wa mavazi bungeni.

Hayo yamesemwa leo Juni 11, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu, wakati wakiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.

 
Dunia inajua Tanzania hakuna bunge wala mahakama huru, endeleeni tu.
 
Back
Top Bottom