Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ametoa onyo kali kwa Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga ambapo amesema Jumatatu ijayo, tarehe 3 Aprili, itakuwa ya mwisho kuandamana.
Gachagua amesema hayo huko Malava kaunti ya Kakamega ambako alihudhuria sherehe ya kutoa shukran kwa ajili ya Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo hilo Injenda Malulu.
"Nataka niwahakikishie watu wa Kenya kuwa hakuna atakayeruhusiwa kuharibu mali tena. Serikali sasa itaonesha nguvu yake kamili." Amesema Gachagua.
"Natoa kwa vijana wanaotumika na Raila Odinga kuwa Jumatatu itakuwa siku yao ya mwisho kuharibu na kuiba mali. Ninyi ni wahuni na tutawashughulikia." Ameongeza Gachagua.
Onyo hili la Gachagua linakuja saa chache tu baada ya Raila Odinga kutangaza kuwa maandamano ya Jumatatu ijayo yatakuwa 'Mama wa maandamano ' yote kuwahi tokea Kenya.