Naibu Waziri Biteko kaanza na kutukatia umeme

Naibu Waziri Biteko kaanza na kutukatia umeme

Anaweza kuzunguka kokote....! Maana hatuambiwi kama Yesu alifika Peru wala Beijing, bali habari za Galilaya na Bethlehem lakini Waziri wa Nje, popote anafika!
Yesu amenukuliwa na waandishi wa biblia:

15:24​

Mt 15:24 SUV​

Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

Kondoo wa Tanzania mlitumiwa shetani kwa mujibu wa biblia:

Shetani ni mungu wa ulimwengu huu (2 Wakorintho 4: 4).​

Mwarobaini wa tatizo la kukatika katika hovyo kwa umeme utatokana na kuwepo miondombinu mizuri ya uzalishaji na usambazaji wa nishati hii nyeti. Waziri WA Nishati katika muda mfupi toka apewe dhamana wala hawezi kutoa suluhu ya papo kwa hapo.
Naibu Waziri Mkuu ni Waziri WA Nishati, sasa Leo SAA 12 asubuhi umeme umekatika, hii inaonyesha ni mgao WA umeme. Naomba ulishughulikie Hilo. Na pia Kwa sababu umepewa hukumu la kuratibu, kuna hiki la SGR Vs Manus ya Wabunge wetu na mawaziri , au mpaka DP weldi na hao wafanya biashara wachukue SGR yetu ndio ufanye KAZI.
Na kuna hiki la Bandari jumps DP weldi au tuendeshe wenyewe Kwa kukopa. Hizo nyenzo na upanuzi WA Bandari
Waziri aliyepita alijitahidi mno kuandaa mipango ya muda wa kati na mrefu, lakini wadau walikosa uvumilimu na yeye kuambulia kila aina ya kejeli na majina mabaya. Suala la usambazaji wa uhakika wa nishati hii nyeti linahitaji muda wa kujipanga na ni gharama pia. Vi vyema rukapima mazuri yote yaliyofanyika mpaka hivi sasa kuliko kuangalia zaidi changamoto zilizopo hivi sasa.

Ndiyo! Tunahitaji huduma ya uhakika, lakini mahitaji yetu haya yanaendana na uhalisia na uwezo wa TANESCO katika kuweka uzania mzuri kati ya utashi na ugavi? Ni kanuni ya kawaida ya kibinadamu pale inapobidi kuwa na maamuzi ya,
"Yure mupe, yure mruke"
 
Waziri ndiye anayefanya umeme ukatike?

Kuna wakati tujue nani wa kupewa lawama...
Huelewi chain of command. Kila mmoja anamwajibisha wa chini yake.

Wananchi wanatakiwa kuiwajibisha Serikali, serikali inamwajibisha mtendaji.

Kwa hiyo wananchi kumlalamikia Waziri au Rais umeme ukikatika ni sahihi kabisa. Hawamjui fundi wala mhandisi maana hawakumpa wao hiyo nafasi.
 
Yesu amenukuliwa na waandishi wa biblia:

15:24​

Mt 15:24 SUV​

Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

Kondoo wa Tanzania mlitumiwa shetani kwa mujibu wa biblia:

Shetani ni mungu wa ulimwengu huu (2 Wakorintho 4: 4).​

Vip umeamka na hangover?
Pata supu au kazimue na bia 2
Kichwa kikae sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huelewi chain of command. Kila mmoja anamwajibisha wa chini yake.

Wananchi wanatakiwa kuiwajibisha Serikali, serikali inamwajibisha mtendaji.

Kwa hiyo wananchi kumlalamikia Waziri au Rais umeme ukikatika ni sahihi kabisa. Hawamjui fundi wala mhandisi maana hawakumpa wao hiyo nafasi.

Kwa hiyo umeme kukatika kwa hitilafu ndio iwe sababu ya kuwajibishwa kwa Waziri?

Kuna sababu za kumtoa waziri lakini sio hitilafu ya umeme...
 
Naibu Waziri Mkuu ni Waziri wa Nishati, sasa Leo SAA 12 asubuhi umeme umekatika, hii inaonyesha ni mgao WA umeme. Naomba ulishughulikie Hilo.

Na pia Kwa sababu umepewa hukumu la kuratibu, kuna hiki la SGR Vs Manus ya Wabunge wetu na mawaziri , au mpaka DP weldi na hao wafanya biashara wachukue SGR yetu ndio ufanye KAZI.

Na kuna hiki la Bandari jumps DP weldi au tuendeshe wenyewe Kwa kukopa. Hizo nyenzo na upanuzi WA Bandari
Naibu Waziri Mkuu, pamoja na shughuli zingine za uratibu, ataratibu mgao wa umeme kwa mujibu wa m kataba wake
 
Mitanzania sijui tukoje? Kwahiyo kiukweli kabisa tunaamini mwanasiasa aitwae waziri ndio huwa anakata na kuwasha umeme?

Hizi shule za siku hizi kweli zinafundisha ujinga.
Wewe ndio naona shukeni huko ulifundihwa mjinga maana umelitafsiri kichwa kichwa andiko la mtoa mada

Kwani unadhani na yeye anaaamini kuwa DOTO BITEKO ndiye anakaa kwenye switch pale ana zima na kuwasha umeme
 
Naibu Waziri Mkuu ni Waziri wa Nishati, sasa Leo SAA 12 asubuhi umeme umekatika, hii inaonyesha ni mgao WA umeme. Naomba ulishughulikie Hilo.

Na pia Kwa sababu umepewa hukumu la kuratibu, kuna hiki la SGR Vs Manus ya Wabunge wetu na mawaziri , au mpaka DP weldi na hao wafanya biashara wachukue SGR yetu ndio ufanye KAZI.

Na kuna hiki la Bandari jumps DP weldi au tuendeshe wenyewe Kwa kukopa. Hizo nyenzo na upanuzi WA Bandari
Amekukatia saa ngapi huo umeme
 
Back
Top Bottom