Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NAIBU WAZIRI BYABATO ASHIRIKI MKUTANO WA NISHATI NCHINI NAMIBIA
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ameshiriki Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano kati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Namibia uliofanyika Jijini Windhoek, Namibia tarehe 10 Machi 2023.
Pamoja na mambo mengine Katika mkutano huo kulisainiwa Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Nishati.
Kwa upande wa Wizara ya Nishati, Naibu Waziri Byabato aliambatana na Naibu Katibu Mkuu, Ndugu Athumani Mbutuka na wataalam kutoka Wizara ya Nishati.