Naibu Waziri Exaud Kigahe (Mb) ameshiriki ufunguzi wa Kongamano la Kibiashara kati ya Tanzania na China

Naibu Waziri Exaud Kigahe (Mb) ameshiriki ufunguzi wa Kongamano la Kibiashara kati ya Tanzania na China

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) Kwa niaba ya Waziri Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameshiriki ufunguzi wa Kongamano la Kibiashara kati ya Tanzania na China lililofanyika hoteli ya Golden tulip jijini Dar es salaam.

Kigahe amesema kuwa makampuni kutoka China yaliyowekeza Tanzania yamesaidia kukua kwa uchumi na ajira kwa watanzania hivyo kuja kwa wafanyabiashara hao kutoka jimbo la Shadong la China kukutana na wafanyabiashara wa Tanzania inaenda kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

Kongamano hilo limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo kansela wa masuala ya Uchumi Bw. Chu Kun, Mwakilishi kutoka jimbo la Shadong pamoja na wawakilishi kutoka TANTRADE, TIC na TTCIA ambao walipata fursa ya kueleza fursa na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini Tanzania.

F0JB2fcWIAEHLon.jpg
F0JB3aiWwAAZjvM.jpg
F0JB4KoXgA0jGCu.jpg
F0JB5AzXwAEyWtX.jpg
 
Back
Top Bottom