PreGE2025 Naibu Waziri Katimba aomba viongozi wa dini, Waumini, kuombea Taifa na Uchaguzi 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Zikiwa zimebaki wiki chache kufikia Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025 linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Zainabu Katimba naye ametoa neno.

Naibu Waziri huyo amewaomba viongozi wa dini pamoja na waumini wa madhehebu yote nchini kuliombea Taifa na pia kuombea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, 2025.

1744286083955.jpeg
​
Mheshimiwa Katimba ametoa ombi hilo alipomuwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri Katimba ametoa msisitizo kwa Watanzania wote kuendelea kuilinda amani na utulivu wa nchi uliyopo sasa.

"Tunawaomba sana viongozi wa dini ya Kiislamu na madhehebu mengine, tuweke msisitizo mkubwa katika kuiombea nchi yetu.

"Ni jambo kubwa sana kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kuzingatia misingi ambayo tumejiwekea kwa miaka mingi.

"Tusifanye uchaguzi kuwa sababu ya kuchochea na kuleta mazingira yatakayoharibu amani ambayo nchi yetu imekuwa nayo kwa miaka mingi," amesisitiza.

Kauli ya mheshimiwa Katimba inaungana na Kampuni ya Msama Promotion ambayo inaandaa Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama amesema hadi kufikia Aprili 9, 2025 maandalizi yamefikia asilimia tisini (90%).

Hata hivyo, Msama ameendelea kuwaomba Watanzania wenye nia njema waendelee kujitokeza kudhamini tamasha hilo ambalo litaanzia Dar es Salaam na kusambaa mikoa mingine ya Tanzania.

"Maandalizi yanakwenda vizuri sana. Karibia asilimia tisini. Lakini bado nawaomba wadau na Watanzania wengine mbalimbali waendelee kujitokeza kwa kudhamini tamasha hili ili lifane.

"Litakuwa tamasha la kumwomba sana Muumba wetu atuzidishie amani katika kipindi chote cha Uchaguzi Mkuu. Tupate viongozi waliyotokana na mapenzi yake na pia kutupitisha salama kipindi cha uchaguzi," alisema Msama.
 
Uchaguzi unavurugwa na chama kimoja tu!
Tuache kuhubiri amani badala yake tuhubiri kwanza HAKI!
Kamwe hakuna amani bila haki. Tuache masihara na kuhadaa umma.
 
Maombi ya kinafiki. Unalazimisha maombi kwenye ujinga.
 
Uchaguzi unavurugwa na chama kimoja tu!
Tuache kuhubiri amani badala yake tuhubiri kwanza HAKI!
Kamwe hakuna amani bila haki. Tuache masihara na kuhadaa umma.
Matamasha ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi na kumhusisha Mungu maombi kwa kitu ambacho kinasababishwa na watawala huko ni kumdhihaki Mungu. Yani unapora haki kisha unawaambia watu waombee amani?
 
Aombee yeye na mawaziri wenzake keki wale wenyewe wengine wahangaike kuombea mafisadi yaendelee kufaidi
 
Kanuni ni rahisi sana"ongea machache,usionyeshe upande Bali ule wa jamuhuri pekee"tutavuka Kwa kishindo!!
 
Utauombeaje Uchafuzi, acheni kumtania Mungu.
 
Maombi gani kwa Mungu yupi ya kuiba kura, mnachekesha sana maana ukimtaja Mungu unataja haki. Mungu hawezi pokea maombi ya kinafiki.
 
Zikiwa zimebaki wiki chache kufikia Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025 linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Zainabu Katimba naye ametoa neno.

Naibu Waziri huyo amewaomba viongozi wa dini pamoja na waumini wa madhehebu yote nchini kuliombea Taifa na pia kuombea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, 2025.

Mheshimiwa Katimba ametoa ombi hilo alipomuwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri Katimba ametoa msisitizo kwa Watanzania wote kuendelea kuilinda amani na utulivu wa nchi uliyopo sasa.

"Tunawaomba sana viongozi wa dini ya Kiislamu na madhehebu mengine, tuweke msisitizo mkubwa katika kuiombea nchi yetu.

"Ni jambo kubwa sana kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kuzingatia misingi ambayo tumejiwekea kwa miaka mingi.

"Tusifanye uchaguzi kuwa sababu ya kuchochea na kuleta mazingira yatakayoharibu amani ambayo nchi yetu imekuwa nayo kwa miaka mingi," amesisitiza.

Kauli ya mheshimiwa Katimba inaungana na Kampuni ya Msama Promotion ambayo inaandaa Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama amesema hadi kufikia Aprili 9, 2025 maandalizi yamefikia asilimia tisini (90%).

Hata hivyo, Msama ameendelea kuwaomba Watanzania wenye nia njema waendelee kujitokeza kudhamini tamasha hilo ambalo litaanzia Dar es Salaam na kusambaa mikoa mingine ya Tanzania.

"Maandalizi yanakwenda vizuri sana. Karibia asilimia tisini. Lakini bado nawaomba wadau na Watanzania wengine mbalimbali waendelee kujitokeza kwa kudhamini tamasha hili ili lifane.

"Litakuwa tamasha la kumwomba sana Muumba wetu atuzidishie amani katika kipindi chote cha Uchaguzi Mkuu. Tupate viongozi waliyotokana na mapenzi yake na pia kutupitisha salama kipindi cha uchaguzi," alisema Msama.
Hii akili ya kutegemea maombi imelirudisha nyuma sana taifa...na imani za dini nazo zimekuwa upuuzi tu...mtu dini yake inakataza dhulma lakini haombi uchaguzi utendeke kwa haki....mashetani wakubwa
 
Back
Top Bottom