Naibu Waziri Kigahe aiagiza kampuni ya Mwenga Hdro powe kupeleka umeme vijiji vyote vya Mufindi

Naibu Waziri Kigahe aiagiza kampuni ya Mwenga Hdro powe kupeleka umeme vijiji vyote vya Mufindi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Naibu Waziri wa Viwanda na biashara na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe,ameitaka kampuni ya Mwenga Hydro power kuboresha huduma zake ili kufikisha nishati ya umeme kwa Wananchi wa Vijiji vyote vinavyopaswa kuhudumiwa na mkataba wa kampuni hiyo kwa mujibu wa mkataba.

Wito huo umetolewa na Kigahe kufutia malalamiko ya Wananchi wa vitongoji vya Ngulika,Kimelela,Winome,na Lupeta katika Kijiji cha Cha Mapanda Wilaya ya Mufindi waliolalamikia kampuni kwa utendaji kazi usioridhisha.

Madai hayo ya Wananchi kukosa umeme yamethibitishwa katika taarifa ya maendeleo ya Kijiji hicho iliyosomwa na afisa mtendaji wa kata ya Bw. Deogratius Komba ambaye pamoja na kubainisha changamoto hiyo pia akatumia fursa hiyo kueleza miradi mbali mbali ya maendeleo iliyotekelezwa.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano ya hadhara iliyofanyika kijijini humo Kigahe amekiri kutofurahishwa na na mwenendo wa kampuni hiyo ya Mwenga Hydro power tangu anaingia madarakani mwaka 2020 huku akisisitiza kuendelea kuihimiza ili iboreshe huduma zake.

Katika hatua nyingine Kigahe amewaomba Wananchi kuwa makini na baadhi ya Watu aliowaita kuwa ni Madalali wa siasa ambao tayari wameanza kupita mitaani na kuwanadi Wanasiasa wao na kueleza kuwa Watu hao hawana lengo la kuwaletea maendeleo bali wanafanya kwa maslahi yao binafsi.

Kigahe aliwataka Madalali hao kuacha kufanya siasa nyepesi wangoje kipyenga kipulizwe waingie kucheza na sio kujaribu kucheza gizani kupitia Waimbaji wa nyimbo bila sauti.

"Nimechaguliwa mwaka 2020 kuwa Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini na kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na biashara wa kwanza na nimekuwa nikifanya ziara za mara kwa mara jimboni kwangu kuhakikisha na kuboresha matumaini kwa kutekelezwa miradi mikubwa ikiwemo barabara, maji na afya shida Iko wapi ? Alihoji Kigahe.
1741352522472.png
 
Back
Top Bottom