Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NAIBU WAZIRI KIGAHE: WAJASIRIAMALI WAPEWE ELIMU YA KURASIMISHA BIASHARA
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe amezitaka mamlaka za Serikali zinazosimamia sekta ya biashara nchini kutoa huduma bora na kuwalea wajasiriamali ili waweze kufanya uzalishaji wenye tija na kuongeza ajira hapa nchini.
Akizungumza katika maonesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair, Naibu Waziri Kigahe amezitaka mamlaka za Serikali nchini kuwaelimisha wajasiriamali katika kurasimisha biashara zao huku akionya tabia za mamlaka hizo kuzifungia biashara za wajasiriamali kabla ya kuwafikia.