Naibu Waziri Kihenzile: Abiria laki nne kuhudumiwa kwa mwaka Arusha Airport

Naibu Waziri Kihenzile: Abiria laki nne kuhudumiwa kwa mwaka Arusha Airport

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Screenshot 2024-09-20 at 23-52-58 @wizara_ya_uchukuzi • Instagram photos and videos.png

Naibu Waziri wa Uchukuzi David kihenzile amesema kukamilika kwa jengo la abiria katika kiwanja cha ndege cha Arusha kutawezesha abiria takribani laki nne kuhudumiwa kupitia Kiwanja hicho kwa mwaka.

Kihenzile ameyasema hayo baada ya kukagua maendeeleo ya mradi wa jengo la abiria katika kiwanjani hapo ambao kwa sasa umefikia asilimia 98 na kusema kukamilika kwa jengo hili kutarahisisha utoaji wa Huduma kwa abiria wanaowasili na kuondoka kiwanjani hapo.

"Kukamilika kwa jengo hili kutatua changamoto ya utoaji wa Huduma kwa abiria wanaowasili na kuondoka sababu jengo la kwanza lilikuwa dogo sana , hatuna budi kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuruhusu Uwekezaji huu mkubwa katika usafiri wa anga” amesema Naibu Waziri Kihenzile.

GX7bqf3WoAActxM.jpg

Naibu Waziri Kihenzile ameipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kumsimamia Mkandarasi Zhixin Construction Limited na kuhakikisha jengo hili linakamilika kwa viwango vilivyokubalika kwenye Mkataba.

Aidha, Naibu Waziri Kihenzile ametanabaisha kuwa tayari Serikali kupitia TAA imeshaanza kutekeleza mradi wa kuweka taa za kuongozea Ndege ili kukiwezesha Kiwanja hicho kutoa huduma kwa saa 24.

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanja cha Arusha Godfrey Kaaya amemuhakikishia Naibu Waziri Kihenzile kuwa kazi ndogo ndogo zilizobaki za zitakamilika ndani ya wiki moja na hivyo kuweza kutoa huduma kwa abiria wanaowasili na kuondoka.

Screenshot 2024-09-20 at 23-53-22 @wizara_ya_uchukuzi • Instagram photos and videos.png

Meneja Kaaya ameongeza kuwa katika kuendelea kuboresha huduma na kuongeza mapato Serikali inatarajia kutekeleza mradi wa ujenzi wa Hotel yenye hadhi ya Nyota nne katika kiwanja cha ndege Arusha Mradi utakaotekelezwa kwa ubia kati kushirikisha sekta binafsi.

Soma Pia:
 

Attachments

  • GX7bqf2WwAEMX32.jpg
    GX7bqf2WwAEMX32.jpg
    102.2 KB · Views: 3
  • GX7bqf3XcAAUb0A.jpg
    GX7bqf3XcAAUb0A.jpg
    178.1 KB · Views: 5
  • GX7bqf0W8AAS5LZ.jpg
    GX7bqf0W8AAS5LZ.jpg
    521.7 KB · Views: 3
  • Screenshot 2024-09-20 at 23-53-35 @wizara_ya_uchukuzi • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-09-20 at 23-53-35 @wizara_ya_uchukuzi • Instagram photos and videos.png
    723.7 KB · Views: 5
Back
Top Bottom