Naibu Waziri Kihenzile aongoza safari ya kwanza ya Treni ya Umeme (SGR) Dar - Morogoro Julai 14, 2024

Naibu Waziri Kihenzile aongoza safari ya kwanza ya Treni ya Umeme (SGR) Dar - Morogoro Julai 14, 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kushereheka furaha ya kuanza kwa safari za treni ya mwendokasi (SGR) Dar es salaam - Morogoro leo June 14,2024, amewalipia tiketi abiria wote kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro na wanaotoka Morogoro kuja Dar es salaam kwa safari ya kwanza.

Naibu waziri wa Uchukuzi David Kihenzile ambaye ameongoza safari hiyo amesema Rais amefanya hivyo ili kuonesha furaha yake kwa kuanza kwa safari hiyo ambapo abiria zaidi ya 600 wamesafiri katika treni hiyo leo “Rais Samia ameona ni vizuri Wananchi wafaidi matunda ya Serikali hivyo ameona kila Mtu anaweza kupanda bure kwa siku ya leo kama ishara ya kushangilia ushindi”

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC ) amewataka Wananchi kutunza miundombinu ya reli hiyo Ili kuleta manufaa kwa Wananchi ambapo amemshukuru Rais Samia kwa Kukamilisha ndoto za Watanzania.

Kadogosa amesema wakati Rais Samia akiingia madarakani alikuta ujenzi wa reli hiyo upo chini ya 50% lakini leo tayari kwa asilimia kubwa imekamilika kipande cha kutoka Dar hadi Dodoma ambapo July 25,2024 rasmi safari za Dar es salaam hadi Dodoma zitaanza.


Pia soma: Treni ya Umeme yatumia dakika 114 Dar hadi Morogoro, Wananchi 600 wasafiri
 
Back
Top Bottom