The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti ameiagiza Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Kufanya tathmini ya mashamba ya Serikali ya mifugo yaliyokodishwa kwa wawekezaji na wakiwabaini waliokodisha mashamba hayo kwa wafugaji kutoka nje ya nchi wavunje Mikataba na kufuta umilikishaji wa mashamba hayo.
Mnyeti ametoa agizo hilo Machi 10, 2025 katika ziara yake mkoani Kagera ambapo amesema Serikali haitakuwa tayari kuruhusu wafugaji kutoka nje ya nchi kuingiza mifugo yao kwenye Mashamba hayo.
Mnyeti ametoa agizo hilo Machi 10, 2025 katika ziara yake mkoani Kagera ambapo amesema Serikali haitakuwa tayari kuruhusu wafugaji kutoka nje ya nchi kuingiza mifugo yao kwenye Mashamba hayo.