Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko amwakilisha Rais Samia Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika 2024, Dodoma

Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko amwakilisha Rais Samia Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika 2024, Dodoma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Fuatilia yanayojiri kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika 2024 - Dodoma.

TLS Biteko.jpg

Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko akijibu hoja ya Mawakili kukamatwa wanapotekeleza majukumu yao amesema kuwa Serikali imelichukua hili. Amesema kuwa nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria hivyo itahikikisha TLS wanapokutana mwakani basi hili lisiwe changamoto ya kusemwa sana. Ameongeza kuwa Mawakili hawa wanakuja kuwatetea watu na kama wanavyoitwa maafisa wa mahakama ni muhimu wakapata heshima yao mahala pa kazi ili waweze kutekeleza majukumu yao kama inavyopaswa.

Naibu Waziri Biteko ameongeza kuwa TLS wanalo jukumu la kuchagua viongozi wataoendeleza mshikamano wa chama hicho, watakaokuwa na kiu na wakati mwingine kuikosoa Serikali, viongozi ambao watakuwa na matamko ya kitaaluma.

Ametoa wito wa TLS kuendelea kuwa na msisitizo wa kuendelea kukaa kwenye taaluma yao kama wanasheria na kuendelea kutekeleza majukumu kwa manufaa ya watanzania.

Dkt. Biteko amesema kuwa wanachama wa TLS wana tofauti mbalimbali kuanzia dini, makabila, ushabiki wa mpira nk lakini wanaunganishwa na kitu kimoja ambacho ni taaluma yao ya Uanasheria


 
Tanganyika Law Society mnalo jukumu kubwa kama chama kumchagua kiongozi atakaye endeleza mshikamano wenu na atakayekuwa na nia ya kuishauri hata kuikosoa serikali, jambo ambalo mmekuwa mkilifanya.

"Naamini mtakuwa na viongozi ambao watakuwa na mawazo, ushauri wa kitaaluma lakini nitoe wito kwa TLS kuendelea kuwa na msisitizo wa kukaa kwenye taaluma yenu kama wanasheria"
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Agosti 1, 2024 amemwakilisha Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Miaka 70 wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) inayofanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pindi Chana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, pamoja na Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika.

Kaulimbiu: “Miaka 70 ya kuwepo kwa Tanganyika Law Society”

1722508253913.png


Soma pia:
Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika 2024, Dodoma
 
Tanganyika Law Society mnalo jukumu kubwa kama chama kumchagua kiongozi atakaye endeleza mshikamano wenu na atakayekuwa na nia ya kuishauri hata kuikosoa serikali, jambo ambalo mmekuwa mkilifanya.

"Naamini mtakuwa na viongozi ambao watakuwa na mawazo, ushauri wa kitaaluma lakini nitoe wito kwa TLS kuendelea kuwa na msisitizo wa kukaa kwenye taaluma yenu kama wanasheria"
Vyovyote vile itakavyokuwa Adv Mwabukusi is the Best Candidate so far
 
TLS YATAKIWA KUSIMAMIA HAKI NA AMANI KUCHOCHEA MAENDELEO

📌 Dkt. Biteko amwakilisha Rais Samia kufungua Mkutano Mkuu 2024

📌 Awataka Mawakili kuchaguana kwa haki

📌 Wananchi zaidi ya 7358 wamefikiwa na TLS kupata huduma

📌 TLS wampongeza Rais Samia kuundwa kwa Tume ya Haki Jinai

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mawakili kusimamia Haki na Amani nchini ili kuhakikisha haki inatendeka kwa watu wote ili kuchochea maendeleo.
IMG-20240801-WA0030.jpg

Dkt. Biteko ametoa wito huo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wanansheria Tanganyika (TLS) kinachoendelea Jijini Dodoma.

" Amani ili iwepo ni lazima haki ionekane ikitendeka kwa maana kwamba haki huleta amani na amani huleta maendeleo kwa nchi yetu," amesema Dkt. Biteko.

Amesema TLS wakati inaadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake, wanachama wake wanatakiwa kutafakari mwelekeo wa chama hicho kitaaluma ili kuendana na azma ya Serikali ya awamu ya sita ambayo imeweka nia thabiti katika kuhakikisha haki inaonekana ikitendeka.
IMG-20240801-WA0032.jpg

“Tumieni muda kusema na kusikiliza hoja za watu wanaojua na wasiojua kwa kuwa nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha kuna heshima mahala pa kazi”. alisema Dkt. Biteko

Aidha Dkt. Biteko amewataka wanachama wa TLS kutumia taaluma yao kushikriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwakani.
IMG-20240801-WA0039.jpg

Awahimiza kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuleta maendeleo badala ya kuzingatia tofuati nyingine zinazowatofutisha binadamu.

Akizungumzia uchaguzi ndani ya TLS, Naibu Waziri Mkuu amewataka wajumbe kuchaguana kwa kuzingatia vigezo nia na mwelekeo wa wagombea watakao kiwezesha chama hicho kusonga mbele na siyo wale wanaotanguliza maslahi binafsi badala ya chama.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameipongeza TLS kwa ushirikiano na taasisi za elimu na taasisi rafiki na TLS kuhakikisha Wananchi wanapata haki kwa wakati.

Amesema Wizara imeanzisha namba maalum inayotumiwa na watu wote kuwasilisha hoja na kuomba ushauri wa kisheria suala linalorahisha upatikanaji wa haki.

Naye, Rais wa TLS Wakili Harold Sungusia amesema kwa sasa katika kitabu cha orodha ya mawakili kuna idadi ya mawakili 12,471 kwa ongezeko hili Watanzania watapata fursa nyingi ya kuhudumiwa na mawakili hawa nchi nzima ili kutatua changamoto zilizopo za kisheria.
IMG-20240801-WA0034.jpg

“ Vitendo vya kukamatwa kwa mawakili hadharani wakati wakiwakilisha wateja wao vimepungua sana ikilinganishwa na miaka iliyopita, tunatamani useme neno mheshimiwa mgeni rasmi ikiwezekana kwa kuwa ni aibu wakili kushikwa Tanganyika Jeck akiwa kazini” amesema Sungusia.

Aidha amepongeza falsafa ya R4 za Mheshimiwa Rais ambazo amesema zimechangia katika kuboresha uhusiano kati ya Wanasheria na mifumo ya usimamizi wa sheria nchini.
IMG-20240801-WA0037.jpg
 
Back
Top Bottom