Naibu Waziri Mwakibete atoa pongezi kwa Chuo cha Bahari (DMI)

Naibu Waziri Mwakibete atoa pongezi kwa Chuo cha Bahari (DMI)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete (MB), amekipongeza Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa kuendelea kutoa mafunzo ya Ubaharia kwa maendeleo ya Uchumi wa Bluu.

Mhe. Mwakibete amesema hayo alipotembelea kwenye banda la Chuo cha Bahari Dar es Salaam kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale vilivyopo Jijini Mbeya.

Chuo cha Bahari Dar es Salaam kinashiriki katika maonesho ya Nanenane 2023 jijini Mbeya ambapo huduma mbalimbali zinatolewa katika banda lao zikiwemo kutoa elimu ya ubaharia, elimu ya uokozi wakati wa dharula melini pamoja na usajili kwa wanafunzi wanaohitaji kujiunga na chuo.

WhatsApp Image 2023-08-03 at 16.09.51.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-03 at 16.09.53 (2).jpeg
WhatsApp Image 2023-08-03 at 16.07.01.jpeg
 
Back
Top Bottom