Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwanaidi Khamis amesema Serikali inaendelea kuelimisha jamii kuhusu sheria za ulinzi wa mtoto ambapo wazazi wasiolea na kutunza watoto adhabu ni faini isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo miezi sita au vyote kwa pamoja.
Akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Najma Giga aliyetaka kufahamu mkakati wa Serikali wa kulinda haki za watoto kutokana na ongezeko kubwa la uvunjifu wa haki za watoto nchini leo Aprili 22, 2025 bungeni Jijini Dodoma, Mwanaidi amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati ya ziada ya kulinda haki za watoto nchini ikiwemo;
Kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa 2024-2029 unaolenga kutokomeza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2029.
Kuendelea kuibua kampeni za kuelimisha jamii kuhusu haki za watoto mfano Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia (2023-2025).
Pamoja na kuimarisha Kamati za Ulinzi wa Mtoto kwenye jamii pamoja na Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto kwenye shule za msingi na sekondari.