Naibu Waziri Mwinjuma atembelea Kituo cha Michezo Tanga na kukutana na makocha waliopo mafunzoni

Naibu Waziri Mwinjuma atembelea Kituo cha Michezo Tanga na kukutana na makocha waliopo mafunzoni

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amewatembelea Makocha ambao wapo kwenye mafunzo ya ngazi ya Diploma ya Ualimu wa Michezo Daraja A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) yanayoendelea katika Kituo cha Michezo Tanga kinachosimamiwa na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF).

Naibu Waziri Mwinjuma amefanya ziara hiyo Juni 12, 2023 jijini Tanga na kukutana na Waalimu hao na kuwasisitiza kutumia fursa hiyo vema ili kujiongezea maarifa ambayo yatasaidia kuinua michezo nchini na kuibua vipajji vya wanamichezo katika maeneo wanayotoka.

Naye Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania Bw. Wales Karia amesema Kozi hiyo ni ya juu na inatambuliwa na CAF na Tanzania ni nchi iliyopewa heshima ya kutoa mafunzo hayo.

Kwa upande wake mmoja wa walimu ambao wanapata mafunzo hayo Bw. Juma Kaseja kutoka timu ya Kagera Sugar amesema mafunzo hayo ni mazuri, wanapata elimu ya juu katika mpira wa miguu Afrika ambayo wataitumia kwa manufaa ya timu wanazofanya kazi pamoja na Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Mafunzo hayo yanawahusisha walimu wa mpira kutoka Zambia, Zimbabwe, Rwanda, Somalia na wenyeji Tanzania.View attachment 2655166View attachment 2655165View attachment 2655167View attachment 2655168View attachment 2655172View attachment 2655169View attachment 2655170View attachment 2655171
IMG-20230612-WA0457.jpg
 
Back
Top Bottom