Naibu Waziri Mwinjuma azungumza na Tamriso na Tuma

Naibu Waziri Mwinjuma azungumza na Tamriso na Tuma

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amekutana na kufanya mazungumzo na Kampuni ya kukusanya na kugawa Mirabaha (TAMRISO) pamoja na Viongozi wa Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya (TUMA).

Mhe. Mwinjuma amekutana na wadau hao leo Agosti 10 2023 jijini Dar se salaam, kwa ajili ya kuona maendeleo yaliyofikiwa na kampuni hiyo ya kugawa mirabaha ambayo ilipewa Leseni na Mamlaka ya kukusanya mirabaha siku chache zilizopita.

Amewahakikishia kuwa, Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali ambazo wameziwasilisha kwake na ambazo zimekuwa zikiwasilishwa mara kwa mara Serikalini.

Kwa upande wao, TAMRISO wamewasilisha taarifa kuhusu utekekezaji wa majukumu waliyopatiwa tangu wakabidhiwe kazi hiyo, ambapo Mhe. Mwinjuma amewataka kuharakisha mambo yaliyobakia ili waanze kukusanya mirabaha na wahakikishe mchakato unafanyika kwa usahihi, ili kuondoa kasoro na malalamiko mbalimbali ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na wadau wa muziki.

IMG-20230810-WA0138.jpg
 
Back
Top Bottom