Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kigoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba amewaomba wanawake wa Mkoa wa Kigoma kuendelea kuhamasika na matumizi ya Nishati safi ya kupikia kwani waathirika wakubwa wa matumizi ya Nishati isiyo rafiki ni wanawake.
Mhe. Katimba amesema hayo wakati akigawa mitungi 200 ya gesi kwa akina mama wa mkoa wa Kigoma ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa
Nishati safi barani Afrika.
Zoezi hilo la ugawaji wa mitungi hiyo ya Gesi limefanyika wilayani Kasulu mara baada ya mafunzo ya matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi na watendaji wa mkoa wa Kigoma iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimmu (NBS) ambapo moja ya wasilisho ni takwimu ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia.
“Mitungi hii ya gesi mtaichukua ninyi ili mkawe mabalozi muende mkahamasishe wanawake wengine na wananchi wote tuunge mkono kampeni ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Tanzania tunatumia Nishati safi ya kupikia na sote tunafahamu nishati isiyo safi inaleta athari na waathitika wakubwa ni akina mama kwasababu sisi akına mama ndio tunashughulika na mambo ya jikoni kwahiyo tunahangaika na moshi wa kuni na mkaa” amesema
Soma Pia: Wananchi Dodoma Jiji Wagawiwa Majiko ya Gesi 1,000 Kuunga Mkono Nishati Safi