Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema sheria na kanuni ya Leseni ya Usafiri wa Umma inamruhusu abiria kupakia mzigo ambao upo chini ya kilo 20 bila kulipia kwenye basi la abiria.
Akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Anatropia Theonest aliyetaka kufahamu ni kwa kiwango gani abiria wanafahamu haki zao wanapotumia usafiri wa umma, Kihenzile amesema kanuni hiyo pia inafanya kazi kwenye treni ya Reli ya Kisasa (SGR) ambapo abiria mwenye mzigo wa chini ya kilo 20 hatakiwi kulipia nauli mzigo wake kwa daraja la uchumi na kilo 30 kwa daraja la biashara.
Hayo yamejiri leo Aprili 22, 2025 bungeni Jijini Dodoma, wakati wa Kipindi cha Maswali na Majibu.