Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amechangia Mizinga 100 ya Nyuki (Milioni 10) na Mitungi ya gesi 150 (Milioni 12,750,00) kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Sengerema kwa lengo la kuwainua kiuchumi na fedha taslimu shilingi milioni 4.5
Hafla hiyo imefanyika Machi 28, 2023 katika Ukumbi wa Wajasiriamali Wilayani Sengerema ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Senyi Ngaga.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ina mkakati wa kuhamasisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati chafu ya mkaa na kuni, hivyo ugawaji wa majiko ya gesi ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kutunza mazingira.
Nishati ya gesi itawasaidia wajasiriamali hao kuepukana na magonjwa ya mapafu na matatizo ya macho yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa katika kupikia.
“Serikali imefanya utafiti na kugundua takribani watu elfu 33 kila mwaka wanapata changamoto ya magonjwa ya mapafu, upofu na kuwa na macho mekundu inayotokana na moshi wa mkaa pamoja na kuni”
Serikali inaendelea kuelimisha wananchi kwamba matumizi sahihi na salama ni kutumia nishati safi ikiwa pamoja na nishati ya gesi na jua.
Kuhusu mizinga ya nyuki, nimewataka wanawake hao kutafuta eneo maalum la kuiweka mizinga hiyo kwa ajili ya kuanzisha biashara ya urinaji wa asali, ambapo pia utasaidia upatikanaji wa nta na maziwa ya nyuki.
Naishukuru Kampuni ya ORYX na FOMAC Kwa ufadhili wao kufanikisha zoezi zima la kuwezesha wajasiriamali.
Nimetoa fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 4,500,000 ambapo kila mjasiriamali alipata shilingi elfu 30. Kwa ajili ya kujaza tena Gas ikiisha.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wananchi Wajasiriamali wadogo wadogo, vijana na wenye walemavu.