Naibu Waziri wa Afya Dkt Ndugulile: Ni marufuku Hospitali kushikilia maiti kwa kile kinachotajwa hadi pale gharama za matibabu yake zitakapolipwa

Naibu Waziri wa Afya Dkt Ndugulile: Ni marufuku Hospitali kushikilia maiti kwa kile kinachotajwa hadi pale gharama za matibabu yake zitakapolipwa

Mkuu wewe ni Master wa maswali nmeamimia fact yako Kuna raia watauwa ndugu zao ili kukwepa gharama heb just imagine mtu anadaiwa 5 mil at hospital nae ndg zake wasilipe achen hzo
Inabidi walipe maana hatujapenda afariki ndio maana madaktari wakawa wanahangaika na mgonjwa,
 
Sure hata mimi hili swala huwa linaniumiza sana. Nadhani serikali kupitia wizara ya afya wangekaa kuangalia tena hili
 
Hili swala ni gumu sana hata mimi linaniumiza ila kuna namna inabidi ifanyike, naomba tujadiliane kwa mtindo wa swali?? Mimi na ww ikiwa tuna hospital na tukapata wagonjwa 20, ndani ya mwezi bahati mbaya wakafariki na wamehudumiwa na madaktari wetu na huduma zetu, na dawa ambazo tumezilipia, haitokua hasara?? Kama jibu ni ndio, serikali ifanyaje kwa waliofark???
Mbona nchi nyingine za Afrika mgonjwa akifariki, maiti inatolewa hospitali, inaenda kuzikwa na deni la hospitali linafutwa?
 
Hapo ndio utaelewa umuhimu wa bima ya afya. Pia kwenye nchi nyingi haswa zilizoendelea bima ya afya ni lazima sio option ili kuepusha mambo kama haya.

Nakupa mfano mdogo sana ili uelewe ulichouliza hakina mashiko

Hospitali mgonjwa anapoletwa kuna gharama zinaingiwa mfano kumpima, kumpa madawa, kumfanyia operesheni, kumlaza, kumhudumia nk. Zile gharama zote zinaingiwa na hospitali ambapo mwisho wake inabidi achangie kwa kuwa kazi ya hospitali sio kutoa msaada bali kutoa huduma kwa gharama zinazohusu huduma hizo

Madawa yanayotumika mahospitalini yananunuliwa na hospitali husika, madaktari wanalipwa, miundo mbinu inakarabatiwa, magari kama ambulance yanawekewa mafuta na kuhudumiwa. Hizo zote ni gharama inaingia hospitali kabla ya kukuletea invoice ya malipo.

Kwa mgonjwa akifa inabidi gharama zilipwe maana huwezi kusema hasara iingie hospitali wakati aliyepata matibabu ni mgonjwa.

Ni sawa na mwanafunzi anayeenda shule akapata huduma zote say kalala boarding, kala chakula, kafundishwa nk halafu siku akifeli mzazi ukadai ada yako kwa kuwa tu akufanikisha lengo.

Tofauti ya mgonjwa na mwanafunzi ni kwamba mgonjwa bill inakuja baada ya matibabu kukamilika

SIJUI NIMEELEWEKA?
 
Kuhudumia watu wanaoelekea kufa ni gharama sana. Sasa zile pesa za dawa nk ambazo hospitali imetumia zitarudije? Si itafilisika.
 
Hospital haitumii dawa za msaada au bure, wanatumia gharama. Mgonjwa huwa hajihudumii wapo wanaomuhudumia, kwa muktadha huo maiti haijihudumii, waliohusika na mgonjwa walipe hakuna jinsi!
Hizi hospital zinalipa mishahara, zinalipa umeme, zinalipa maji, zinaboresha majengo n.k.
TULIPE! Nilidaiwa alipofariki mama mzazi nikapaniki lakini Director alinielewesha nikajiona fala. Tukajichanga tukalipa walitupunguzia kidogo, gharama za kitanda.

Ila tulipe ili hizi hospital ziweze kujiendesha, na kutuhudumia tulio hai.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mbona nchi nyingine za Afrika mgonjwa akifariki, maiti inatolewa hospitali, inaenda kuzikwa na deni la hospitali linafutwa?
Wapi huko?
Public hospital au private hospital au hospital yoyote?

Everyday is Saturday................................😎
 
Mahakama si zipo?
Wafunguliwe mashtaka
Wapewe dhamana au
Waende rumande, hao marehemu
 
Back
Top Bottom