Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile aelezea aina za Barakoa za kuvaa na Utaratibu wa kutengeneza ya kitambaa

Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile aelezea aina za Barakoa za kuvaa na Utaratibu wa kutengeneza ya kitambaa

Kutokana na umuhimu wa barakoa jifunze hapa namna ya kutengeneza barakoa rahisi

 
Mbona mnatuchanganya sana! hivi Serikali hii ni yupi ambae tunapashwa tumsikilize? Na yupi ambae ni msemaji wa Serikali juu ya maswala ya kitalamu kuhusu Corona? Je Makonda kwenye mkoa anao uongoza hana watalamu na wenye akili za kushindwa kuwatumia Katika kipindi hiki kigumu,ukiacha na Waziri je RMO wa Dsm anakazi gani? Au Makonda anakaimu nafasi ya RMO.
Soma Naibu Waziri kasema nini hasa hapo mwisho alivyomalizia, nadhani hutoumiza kichwa tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kila barakoa ni barakoa!
255715518850_status_fe7867bd0a6f4168961ba0fd4d6d906d.jpg


The good, the bad and the ugly.
 
Mbona mnatuchanganya sana! hivi Serikali hii ni yupi ambae tunapashwa tumsikilize? Na yupi ambae ni msemaji wa Serikali juu ya maswala ya kitalamu kuhusu Corona? Je Makonda kwenye mkoa anao uongoza hana watalamu na wenye akili za kushindwa kuwatumia Katika kipindi hiki kigumu,ukiacha na Waziri je RMO wa Dsm anakazi gani? Au Makonda anakaimu nafasi ya RMO.
Hatamie najiuliza, akipigwa risasi jambazi kwenye majibizano anaetoa taarifa/ufafanuzi Ni mambosasa na sio mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa, Ila hili la corona RMO hatumsikii kabisa badala yake mwenyekiti wa ulinzi na usalama ndio kunara, Kama ndio hivyo Basi masuala yote yahusuyo mkoa yazungumzwe na mtu mmoja, kuanzia idadi ya majambazi Hadi corona
 
Makonda yuko sahihi.
Ni bora kuvaa barakoa ya kitambaa.
Lesso ikikunjwa vizuri inazuia Corona kusambaa .
Na pia kitambaa ni rahisi kukifua kwa sabuni na maji ya moto na kukipiga pasi kwa wale wasio na Sh.3000 /- za Maski ya kitabibu inayonunuliwa kila siku na kuibadili kila baada ya masaa manne.

Huyo waziri atakua na mafamasi mengi na amelenga kufanya biashara.
Ubinafsi wa mwanadam ndio ulioleta Corona kwa manufaa ya kiuchumi zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wote wako sahihi mkuu, waziri kasema kutumia kitambaa cha pamba kwa wale ambao hawana uwezo. Ni ushauri mzuri

Tatizo watanzania tumezoea kushikiwa akili zetu. Watu wana access za internet lakini wavivu wa kutafuta mambo muhimu mpaka waambiwe na serikali.

Hivi kweli mpaka leo hatujui umuhimu wa kuvaa barakoa au masks mpaka serikali itoe amri?

Mnashindwa kutafuta jinsi ya kutengeneza masks au kusoma masks gani zinafaa kutoka vyombo vya uhakika kama WHO na vingine?

Tuache mzaa, tujifunze kutoka kwa wenzetu hili tupunguze maambukizi.

Ushauri wako mzuri na ni rahisi kusoma labda wataelewa. Wako busy kumshambulia Makonda, kuna wakati chuki binafsi tunatakiwa tuweke pembeni.
 
Acheni kupotosha watu, barakoa za vitambaa bado zina msaada, hata nchini ujerumani watu wameambiwa wanaweza kuzitumia, ukifuata kiki za hao wanasiasa utapotea. Kwa akili ya kawaida ni asilimia ngapi ya watu wanamudu kutumia N95 ukizingatia kwamba matumizi yake ni ndani ya siku moja. Wanasiasa wanaoleta utaalamu uchwara kwenye swala serious la korona ni bora rais angeanza nao mapema kabla hawajasababisha majanga zaidi...
Wanasiasa wanaingilia mambo ya kitaalam
Wana wapoteza tu watu

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pua na midomo zimegeuka sehemu za siri, ajabu sana hii.

Corona is overrated.
 
Wanasiasa wangekaa kimya ktk kipindi hiki Cha Corona...

Makonda kauli zake zinamfanya aoneoane Ni mtu wa kukurupuka tu kwa matamko yasiyo tekelezeka...
Wengi wenu mna chuki binafsi na Makonda, lakini mjue Makonda bado yupo yupo sana!
 
Back
Top Bottom