Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile atenguliwa, Godwin Mollel achukua nafasi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
DKT FAUSTINE NDUGULILE ATENGULIWA



Rais John Pombe Magufuli amemtengua Dr Faustine Ndugulile Naibu Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mbunge wa Kigamboni.

Nafasi hiyo imechukuliwa na Dkt Godwin Mollel, Mbunge wa Siha, aliyeteuliwa Mei 16 kushika nafasi ya Dkt Ndugulile

Uteuzi wa Dkt Mollel unaanza Mei 16, 2020

Faustine aliteuliwa 07 Oktoba 2017 akichukua nafasi ya Khamis Kigwangala aliyeenda kuwa Waziri wa Utalii

Tarehe 14 Des 2017, Mbunge wa Jimbo la Siha, Dk. Godwin Mollel alihama chama cha CHADEMA na kujiunga CCM.

Zaidi, soma

1). Tumwamini nani kati ya Rais Magufuli au Daktari Ndugulile kuhusu kujifukiza ili kukabiliana na COVID-19? - JamiiForums

2). Hongera Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri wa Afya - JamiiForums



Maoni ya Ndugulile kuhusiana na ugonjwa wa Corona:


Mchango wa Mollel bungeni:

 
Ndungulile alitaka sayansi itawale na sio ujinga wa nyungu sijui kujifukiza ambako hakuna ushahidi wa kisayansi kama kunatibu ugonjwa. Hii iko kinyume na matakwa ya boss anaetaka ujinga ndio utumike kama tiba ya corona.

Ndungulile hakupigia debe matakwa ya bosi wake ya kutumia tiba za kienyeji.

Kwenye kitabu cha Robert Greene cha 48 rules of power, Rule namba moja inasema never out smart your master. Always make them feel or appear more brilliant than he is. Always make your boss feel intelligent than you.

Ndugu yangu Ndungulile utakua ulisahau hili.
 
Rais John Pombe Magufuli amemtengua Dkt Faustine Ndugulile, aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Nafasi hiyo imechukuliwa na Dkt Godwin Mollel, Mbunge wa Siha, aliyeteuliwa Mei 16 kushika nafasi ya Dkt Ndugulile

Uteuzi wa Dkt Mollel unaanza Mei 16, 2020

 
Kanywe nae chai,imetoka hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli bwana naona ana masihara sana. Ile kamati ya Ummy kumbe Prof. Lyamuya alijiuzulu uenyekiti na akajiondoa kamatini. Serikali hii ni ya ajabu sana sana.

Ndugulile amejiuzulu asitudanganye hapa!
Kwanini alijiuzuru mkuu?
 
Mikono juu!! Haya twende ukaeleze vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa na "layman" kwenye masuala nyeti harafu mbishi, mjeuri na mwenye ego kubwa kuliko kichwa chake, ni tatizo.

Dr. Ndungulile alipinga huo ujinga wa kupropagate the so called nyungu bila facts (miti ipi, kiasi gani, ujifukize dakika ngapi etc). Pia alipinga mambo ya barakoa za kushona. Kiufupi alikuwa anampa shule Jiwe na kwa Jiwe hilo ni kosa kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…