Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence George, ameeleza bungeni leo Septemba 2, 2026 kuwa serikali inaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ili kuhakikisha kila mwananchi anapata na kumudu huduma za afya nchini.
“Serikali inasimamia utekelezaji wa bima ya Afya kwa wote ambapo hadi Juni 2026 jumla ya kaya 276,004 sawa na asilimia 100 ya kaya maskini zilizolengwa kugharamiwa na Serikali kwa awamu ya kwanza zimesajiliwa, na jumla ya wanufaika milioni 1.4 wamegharamikiwa bima ya afya na Serikali.”