Pre GE2025 Naibu Waziri wa ardhi, Geoffrey Pinda: Watumishi wa ardhi msiyumbishwe na misimamo ya kisiasa

Pre GE2025 Naibu Waziri wa ardhi, Geoffrey Pinda: Watumishi wa ardhi msiyumbishwe na misimamo ya kisiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Geoffrey Pinda, amewataka watumishi wa ardhi nchini kuacha kuyumbishwa na misimamo ya kisiasa, badala yake wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kusimamia sheria na kutoa maamuzi sahihi kuhusu migogoro ya ardhi.

Pia amesisitiza kuwa kushindwa kutoa taarifa za ukweli kwa viongozi wanaotafuta suluhisho la migogoro hiyo, kumechangia kucheleweshwa kwa maamuzi muhimu, hali inayowaathiri wananchi moja kwa moja kupata haki zao.

Pinda amebainisha hayo leo Jumanne, Februari 25, 2025, akiwa mkoani Morogoro wakati akifungua kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa ardhi kutoka wilaya zote tisa za mkoa wa Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya kliniki ya ardhi inayofika tamati Machi 01, 2025.

 
Back
Top Bottom