Mpepetaji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 346
- 213
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema utekelezaji wa ujenzi wa daraja la Mitomoni lenye urefu wa mita 80 umefikia asilimia 21 unatekelezwa kupitia fedha za dharura zilizotolewa na bank ya dunia kupitia dirisha la Contigency Emegency response component (CEC)kwa gharama ya shilingi bilioni 9.29 ambapo mkataba wa mradi huo ulisainiwa November 2024 na unatarajia kukamilika mwezi September 2025
Naibu Waziri amezungumza hayo jana bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mh.Mbunge wa Viti Maalum Jacline Ngonyani wa mkoani Ruvuma aliyeuliza “Ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa daraja la mitomoni”
“Mh.Naibu Spika nimhakikishie Mh.mbunge mikataba yote tuliyosaini na tulivyokubaliana na wenzetu wa world bank miradi yote inatakiwa ikamilishwe ndani ya mwaka mmoja na hatutegemei kuwa na changamoto yeyote ya mtiririko wa fedha tulishakubaliana na wakandarasi tunawasimamia na kuhakikisha wanakamilisha kazi kama tulivyokubaliana kwenye mkataba,”Amesema Kasekenya
Aidha Ngonyani ametoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo kubwa na la kimkakati lililokua linasababisha adhari kwa wananchi wa eneo hilo,
Daraja la Mitomoni linaunganisha Wilaya ya Nyasa na Songea Vijijini utekelezaji wake ukikamilika utachochea shughuli za kiuchumi pamoja na usafiri na usafirishaji.