Naibu Waziri wa Utalii akiri ni kweli bila vivutio kutangazwa utalii hauwezi kuendelezwa

Naibu Waziri wa Utalii akiri ni kweli bila vivutio kutangazwa utalii hauwezi kuendelezwa

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amekiri bila kutangaza vivutio vilivyopo nchini Utalii hauwezi kuendelezwa. Ametoa kauli hiyo akimjibu Mbunge aliyehoji kuhusu mkakati wa kutangaza vivutio vya Kusini.

Akiwa Bungeni, Masanja amesema bila kuimarisha miundombinu utangazaji wa vivutio ni changamoto. Ameeleza Bilioni 46.5 zimetengwa kuhakikisha utangazaji unafanyika kwa nguvu. Pia Bilioni 75.4 zimetengwa kuimarisha miundombinu.
 
Ahsante kwa Taarifa, ila ni kwanini ukishaleta Taarifa kama hii hurudi tena tujadili kwa pamoja zaidi ya kutokomea kusikojulikana..,
Si unajuwa Michango yetu kwenye haya mambo ya Utalii inaweza kusababisha tutishiwe lakini!!!
 
Kwani kituo kikuu cha utalii kanda ya ziwa pale Chato panaendeleaje?
 
Bila kufuata protocols za WHO kuhusu covid19 ni kazi bure Tanzania itakuwa stigmatized, mtakuwa "Lockedin", mtapata watalii backpackers wasio na pesa maana wenye pesa ni wastaafu na middle class ambao wako vurnerable kuambukizwa covid19.
 
21 January 2021
Zanzibar

Episode 1:Siri ya utalii Zanzibar(The secret of tourism in Zanzibar)Katibu mtendaji mstaafu aelezea.


Mzee Walid Fikirini Silima, Katibu mtendaji mstaafu wa kwanza kamisheni ya utalii akielezea wazi wazi siri ya utalii ya Zanzibar kufanya vizuri .

Mzee Silima anabainisha aina kadhaa za utalii . Vipi utalii ulianza na vipi utalii ulikua kabla na hivi sasa ulivyo utalii ndani ya Zanzibar. vilevile ameelezea vingi sana kuhusu utalii, usiache kufatilia vipindi hivi ili ufahamu kwa kina tulipotoka tulipo na tunapokwenda katika swala zima la utalii.
Source : Dhow TV
 
Back
Top Bottom