PostGE2025 Naibu Waziri Wanu aagiza kozi fupi zilizositishwa VETA zirejeshwe

PostGE2025 Naibu Waziri Wanu aagiza kozi fupi zilizositishwa VETA zirejeshwe

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, amevitaka vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) nchini kurejesha kozi za muda mfupi za kilimo na ufugaji zilizokuwa zimesitishwa, ili kuwawezesha Vijana kupata ujuzi unaoendana na mahitaji ya maeneo yao na kujiajiri baada ya kuhitimu.

Wanu ametoa maelekezo hayo leo, Novemba 26, 2025, wakati wa ziara yake katika Chuo cha VETA Chemba, ambapo pia alizindua ugawaji wa vifaa vya mafunzo kwa Vyuo 63 vya VETA nchini kwa Kanda ya Kati.

View attachment 3507890

Amesema VETA ni taasisi muhimu na ya kimkakati katika kuchangia utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya nchi, hususan katika kukuza uchumi kulingana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku akivielekeza vyuo hivyo kujikita katika kutoa mafunzo yanayochochea matumizi ya TEHAMA, ikiwemo Akili Mnemba (AI) na teknolojia ya roboti, ili kuendana na mahitaji ya Uchumi wa Kidijitali.

Wanu amesema Tanzania inaendelea kupiga hatua katika Sekta ya Viwanda na Uchumi, huku maeneo ya uwekezaji yakiongezeka kufuatia ujenzi wa viwanda vikubwa na vya kati. Amesisitiza kuwa mafanikio hayo yanahitaji nguvu kazi yenye ujuzi na maarifa ya kutosha.

Aidha, amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha VETA inapatiwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya mafunzo, na kuiagiza taasisi hiyo kuzingatia ubora wa utoaji wa elimu ili uendane na mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Huyu ni kilaza kama bimkubwa wake tu apuuzwe
 
NW WANU ASISITIZA VETA KUWEKEZA KATIKA TEHAMA, AKILI UNDE NA ROBOTI ILI KUKUZA UCHUMI KIDIGITALI

Wilaya ya Chemba yapokea Shilingi Bilioni 1.83 Sekta ya Elimu kutoka Serikalini

Naibu Waziri Wanu Ameir azindua ugawaji wa vifaa vya Mafunzo ya Ubunifu, Ushonaji, Teknolojia ya Nguo na Umeme kwa Vyuo vya VETA 63 nchini

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imezindua ugawaji wa vifaa vya mafunzo ya ubunifu, ushonaji, teknolojia ya nguo na umeme kwa Vyuo vya VETA 63 nchini ili kuimarisha utolewaji wa mafunzo ya ufundi stadi na kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Uzinduzi huo umefanywa leo tarehe 26 Novemba, 2025 katika Chuo cha VETA cha Wilaya ya Chemba na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Wanu Ameir amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha VETA inapatiwa vifaa vya kisasa na vya kutosha, pamoja na kuajiri wakufunzi wenye ujuzi na mbinu za kufundishia zinazoendana na wakati.

Mhe. Wanu Ameir Amesema Uimarishaji na ongezeko la Vyuo vya VETA nchini ni utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2024 (Toleo la 2023) kwa kutoa fursa za mafunzo kwa vijana ili kuandaa nguvukazi yenye ujuzi inayohitajika katika uzalishaji kwenye sekta mbalimbali.

Mhe. Wanu Ameir, amesisitiza umuhimu wa VETA kujielekeza katika mafunzo yanayochochea matumizi ya TEHAMA, Akili Unde na Roboti, ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia katika Uchumi wa Kidijitali.

Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema kuwa vifaa vilivyogawiwa ni msingi mzuri wa mafunzo kwa kuwaandaa wanachuo wawe na uwezo wa kutenda kwa vitendo, kufanya kazi kwa pamoja na kujiandaa ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira.

Kwa upande wake, CPA Antony Kassori, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, amesema vifaa vilivyonunuliwa na Serikali vina thamani ya shilingi bilioni saba na vitasambazwa katika vyuo 63 vya VETA. Ameongeza kuwa kwa sasa VETA ina zaidi ya vyuo 80 vyenye uwezo wa kudahili wanafunzi 120,000 kwa mwaka, huku vyuo vingine 65 vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi. Vikikamilika, VETA itakuwa na zaidi ya vyuo 145 vyenye uwezo wa kudahili wanafunzi zaidi ya 250,000 kwa mwaka.

Serikali imeweka bayana kuwa nguvukazi yenye ujuzi na ubunifu ndiyo nguzo ya kufanikisha azma ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati unaotegemea uzalishaji kwa wingi na teknolojia ya kisasa.

Awali, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir aliwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa VETA za Wilaya.

Mhe. Wanu Ameir ameelezwa kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 tayari Wilaya ya Chemba imeshapokea Shilingi bilioni 1.83 kwa ajili ya sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa miundombinu.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipanda Mti katika Chuo Cha VETA cha Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.

#TunaboreshaElimuYetu
#KaziIendelee

 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, amevitaka vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) nchini kurejesha kozi za muda mfupi za kilimo na ufugaji zilizokuwa zimesitishwa, ili kuwawezesha Vijana kupata ujuzi unaoendana na mahitaji ya maeneo yao na kujiajiri baada ya kuhitimu.

Wanu ametoa maelekezo hayo leo, Novemba 26, 2025, wakati wa ziara yake katika Chuo cha VETA Chemba, ambapo pia alizindua ugawaji wa vifaa vya mafunzo kwa Vyuo 63 vya VETA nchini kwa Kanda ya Kati.

View attachment 3507890

Amesema VETA ni taasisi muhimu na ya kimkakati katika kuchangia utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya nchi, hususan katika kukuza uchumi kulingana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku akivielekeza vyuo hivyo kujikita katika kutoa mafunzo yanayochochea matumizi ya TEHAMA, ikiwemo Akili Mnemba (AI) na teknolojia ya roboti, ili kuendana na mahitaji ya Uchumi wa Kidijitali.

Wanu amesema Tanzania inaendelea kupiga hatua katika Sekta ya Viwanda na Uchumi, huku maeneo ya uwekezaji yakiongezeka kufuatia ujenzi wa viwanda vikubwa na vya kati. Amesisitiza kuwa mafanikio hayo yanahitaji nguvu kazi yenye ujuzi na maarifa ya kutosha.

Aidha, amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha VETA inapatiwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya mafunzo, na kuiagiza taasisi hiyo kuzingatia ubora wa utoaji wa elimu ili uendane na mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Hizo kozi ndizo zimemfikisha yeye na mama yake hapo walipo.
 
Aidha, amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha VETA inapatiwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya mafunzo, na kuiagiza taasisi hiyo kuzingatia ubora wa utoaji wa elimu ili uendane na mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Naibu Waziri feki, hii ni serikali ya muda mfupi kweli... viongozi waliosoma kozi fupifupi wamejazwa kwenye baraza la mawaziri.. muda walio nao kua hapo ni mfupi na muda sio rafiki
 
Kwenye wizara ya elimu wangekuwa wanaweka viongozi walioelimika, Tanganyika tunao wasomi wengi sana
Hawa akina Wanu wakawe manaibu waziri wa elimu huko Zanzibar
 
Tz nchi pekee akili ndogo ndiyo anapewa taasisi nyeti aongoze
Yaani mambo bora liende kumsukuma mlevi tu

Ova
 
Back
Top Bottom