Naibu Waziri, Zainab Katimba: Mkandarasi CRJE EAST AFRICA LTD Kamilisha Ujenzi wa Barabara kwa Wakati

Naibu Waziri, Zainab Katimba: Mkandarasi CRJE EAST AFRICA LTD Kamilisha Ujenzi wa Barabara kwa Wakati

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. ZAINABU KATIMBA: MKANDARASI CRJE EAST AFRICA LTD KAMILISHA UJENZI WA BARABARA KWA WAKATI

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Zainab Athman Katimba amemuagiza Mkandarasi M/s CRJE East Africa LTD kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa barabara Wafipa - Kagera na Bangwe- Burega kwa wakati.

Mhe. Zainab Athman Katimba ametoa kauli hiyo Mei 31, 2024 wakati alipokagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata ya Bongwe, Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma.

Mhe. Zainab Athman Katimba Amemtaka Mkandarasi kufuata sheria, taratibu na miongozo iliyowekwa kwenye mikataba ambayo inaeleza wazi barabara hiyo inatakiwa kukamilika lini ili wananchi waweze kupata huduma za usafirishaji.

"Wakandarasi mnapopatiwa kazi jukumu lenu ni kutekeleza kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa kwa kuwa mnapokuwa nyuma ya ratiba mnakwamisha maendeleo ya wananchi"

Aidha, Mhe. Zainab Athman Katimba Amemtaka kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati kwa kuwa wananchi wanamatarajio makubwa na Serikali inahitaji kuona fedha inayotengwa kwa ajili ya ujenzi inaleta matokeo chanya.

Vilevile, Mhe. Zainab Athman Katimba amesema Serikali haitafumbia macho ucheleweshaji wa ujenzi wa miundombinu ya barabara ama kusuasua kwa utekelezaji wa miradi nchini.

Naye, Diwani wa Kata ya Bangwe Mhe. Hamis Besere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya trioni 11 kwa ajili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Kigoma.

Aidha, amewaomba wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo kujenga kwa ubora unaotakiwa na kuikamilisha ndani ya muda wa makubaliano.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-06-01 at 13.22.12.mp4
    10.6 MB
  • GO90V5-XgAArVkq.jpg
    GO90V5-XgAArVkq.jpg
    84.5 KB · Views: 2
  • GO90V_VWUAAd2Vw.jpg
    GO90V_VWUAAd2Vw.jpg
    116.3 KB · Views: 2
  • GO90V8FWwAAirbK.jpg
    GO90V8FWwAAirbK.jpg
    66.8 KB · Views: 3
  • GO90V8IWgAASqhw.jpg
    GO90V8IWgAASqhw.jpg
    66.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom