JF nimeolewa miaka nane iliyopita nikiwa na 21 years old,nimekaa na mme wangu katika ups and down za ndoa ..
Ila mme wangu naona ana mambo mengi ya ujana,dharau na kutojari familia , hakui najaribu kumwelewesha misingi ya ndoa na kumwelewesha pale anapoenda kinyume
lakini inakuwa kazi bure.
Kinachoniuma nadhani nampenda sana mme wangu akinikosea ninaumia hata week nzima siwezi kula ,kulala Napata shida wakati yeye
Anakuwa normal na hana hata muda wa kuomba msamaha.
Nahisi haya mapenzi niliyonayo kwa mme wangu yananiua ama kunipeleka vibaya.
Mtaalam mmoja aliniambia Tatizo langu nina 75% ya penzi kwa mme ,nijaribu kuweka 50/50%
Najitahidi kufanya hivo na ku-ignore yote anayoyafanya ,,mwisho wa siku nashindwa najikuta naendelea kuumia zaidi na kunyongonyea .
Ni mengi anayonikosea.
JF ninawezaje kupunguza haya mapenzi ili niishi kwa Amani?
Nisaidie nakufa siku si zangu..nifundisheni nilipunguze vip hili penzi kwa baba chanja nisiumie
Mama Clea