Naifatilia hii realmotors naona wana Magari mazuri, kuna mtu yoyote alishawahi agiza gari na hii kampuni?

Cash Generating Unit

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
13,286
Reaction score
39,418
Toka nianze harakati za kusaka gari mtandaoni kila gari naona ya kawaida yani nikipata gari zuri bhs inakasoro inanikata mzuka. Nimetembelea web zote za kuimport japani ila sijaridhika.

Toka jana naifatilia hii realmotors naona wanagari nzuri, kuna mtu yyte alishawai agiza gari na hii kampuni?? Na huduma zao zikoje? Manake wengi wanatumia sbt na Beforward.

IMG_0597.jpg

IMG_0596.jpg
 
RMJ wana gari nzuri sana hazina mileage kubwa na bei zao nzuri. Wana gari chache ila nzuri. Niliawahi kuagiza IST nilikaa nayo 3 yrs sikubadili spare zaidi ya tyres. Kuna wakala wao yupo ushirika tower lumumba wanaitwa Afritel ndio walinisaidia kuclear pia. Thou kila kitu nililipa mwenyewe.
 
Ukitaka gari isiyo na kasoro, agiza au nunua NEW BRAND toka kiwandani moja kwa moja uchane karatasi mwenyewe huku ukipata na guarantee/warrant ya mwaka mzima na hata zaidi.

Lakini kama unataka kununua kutoka ktk kampuni hizi zinazo - deal/uza magari yaliyokwisha kutumika (used/second hand), hakuna guarantee kuwa unaweza kupata a complete perfect car with no any defection kwa 100%. Ndiyo maana zinaitwa " used".

Kwa sababu hii, naweza kusema bila shaka yoyote kuwa hakuna kampuni yoyote inayouza USED CARS tunayoweza kusema moja kwa moja ni nzuri sana au ni mbaya sana kwa sababu it depends..

Mathalani, usitegemee hili,kuwa, NOAH NEW MODEL brand new inauzwa hadi Tshs. 100,000,000. Lakini hiyo hiyo ikiitwa "used" inauzwa hadi 15,000,000 mpaka inakuwa mikononi mwako.

Katika scenario hii usitegemee usikute defection kwenye gari ya namna hii hata iwe inang'aa kwa mng'aro mzuri kiasi gani...!!

HATA HIVYO; Mara nyingi kutoka kwenye kampuni hizihizi unaweza kubahatika ukauziwa gari used bora na nzuri kabisa ikiwa na tofauti ndogo sana na aliyenunua BRAND NEW!
 
RMJ wana gari nzuri sana hazina mileage kubwa na bei zao nzuri. Wana gari chache ila nzuri. Niliawahi kuagiza IST nilikaa nayo 3 yrs sikubadili spare zaidi ya tyres. Kuna wakala wao yupo ushirika tower lumumba wanaitwa Afritel ndio walinisaidia kuclear pia. Thou kila kitu nililipa mwenyewe.

Najaribu ku create account RMJ inanigomea shida ni nn?
 
Nimesoma paragraph yako ya kwanza na nikaangalia picha uliopost nimeshindwa kuelewa...yaan gari nyingi za kawaida lakin umepost IST
 
Toka nianze harakati za kusaka gari mtandaoni kila gari naona ya kawaida yani nikipata gari zuri bhs inakasoro inanikata mzuka. Nimetembelea web zote za kuimport japani ila sijaridhika...

Mkuu hongera kwa mchakato huo na hitaji lako la ushauri. Mimi nina uzoefu wa kutosha kuagiza magari kwa kampuni kadhaa.

Ngoja nikupe maoni yangu kuhusu kampuni za magari.

Miongoni mwa kampuni bora ambazo ukiagiza gari una uhakika wa kupata gari nzuri sana ni:

1. Autorec - hawa wana magari mazuri sana ila bei yao ni shida. Sababu ni kuwa kabla hujauziwa gari inafanyiwa reconditioning, nakuhakikishia gari zao ni used ila ni top. Shida ni hapo ktk bei.

2. Trust - Hawa pia wana magari top quality, ni kama autorec na bei zimechangamka kdg.

3. Real Motors - Hawa wanauza gari nzuri sana, kwa maoni yangu, tofauti na autorec na trust wao hawafanyi reconditioning ila wana point gari nzuri tuu. Hivyo bei zao ni cheaper na quality ni nzuri. Kwa kawaida hawapendi kuwa na gari zaidi ya km 100,000.

Shida yao ni moja tu, customer service sio nzuri yaani hawabembelezi mteja kamwe. Nadhani wanauza magari kwa passion na sio kutafuta pesa.

Ushauri: Kati ya kampuni zote hizo kwa kuangalia bajeti ya mtanzania wa kawaida, Real Motors is the best kwa sababu utapata gari nzuri na bei nzuri, hilo la customer care mtavumiliana.
 
HUko kote watauza Magari Ila be forward watabaki kuwa namba 1 kwasabb hawa jamaa wanauza gari ikiwa imepigwa picha hata kama kuna mchubuko mdogo wataonesha yaani kila kasoro ya gari utapewa tofauti na kampuni zote za Magari Japan
 
Hebu jaribu kuwatembelea tradecarview, kwa hawa wajapani hautojuta. Nimeshaagiza gari tatu kwao, wapo vizuri. Uzuri wa hawa jamaa wanakuunganisha na mwenye gari kwaajili ya negotiation wao wanakuwa madalali kwa kamisheni ndogo sana.
 
Mkuu hongera kwa mchakato huo na hitaji lako la ushauri. Mimi nina uzoefu wa kutosha kuagiza magari kwa kampuni kadhaa.

Ngoja nikupe maoni yangu kuhusu kampuni za magari.

Miongoni mwa kampuni bora ambazo ukiagiza gari una uhakika wa kupata gari nzuri sana ni:

1. Autorec - hawa wana magari mazuri sana ila bei yao ni shida. Sababu ni kuwa kabla hujauziwa gari inafanyiwa reconditioning, nakuhakikishia gari zao ni used ila ni top. Shida ni hapo ktk bei.

2. Trust - Hawa pia wana magari top quality, ni kama autorec na bei zimechangamka kdg.

3. Real Motors - Hawa wanauza gari nzuri sana, kwa maoni yangu, tofauti na autorec na trust wao hawafanyi reconditioning ila wana point gari nzuri tuu. Hivyo bei zao ni cheaper na quality ni nzuri. Kwa kawaida hawapendi kuwa na gari zaidi ya km 100,000.

Shida yao ni moja tu, customer service sio nzuri yaani hawabembelezi mteja kamwe. Nadhani wanauza magari kwa passion na sio kutafuta pesa.

Ushauri: Kati ya kampuni zote hizo kwa kuangalia bajeti ya mtanzania wa kawaida, Real Motors is the best kwa sababu utapata gari nzuri na bei nzuri, hilo la customer care mtavumiliana.

Kucreate account tu shida, mpaka sasa nasubiri confirmation email ila bado hawatumii kwahyo mkuu unanishaurije hapo
 
Mkuu hongera kwa mchakato huo na hitaji lako la ushauri. Mimi nina uzoefu wa kutosha kuagiza magari kwa kampuni kadhaa.

Ngoja nikupe maoni yangu kuhusu kampuni za magari.

Miongoni mwa kampuni bora ambazo ukiagiza gari una uhakika wa kupata gari nzuri sana ni:

1. Autorec - hawa wana magari mazuri sana ila bei yao ni shida. Sababu ni kuwa kabla hujauziwa gari inafanyiwa reconditioning, nakuhakikishia gari zao ni used ila ni top. Shida ni hapo ktk bei.

2. Trust - Hawa pia wana magari top quality, ni kama autorec na bei zimechangamka kdg.

3. Real Motors - Hawa wanauza gari nzuri sana, kwa maoni yangu, tofauti na autorec na trust wao hawafanyi reconditioning ila wana point gari nzuri tuu. Hivyo bei zao ni cheaper na quality ni nzuri. Kwa kawaida hawapendi kuwa na gari zaidi ya km 100,000.

Shida yao ni moja tu, customer service sio nzuri yaani hawabembelezi mteja kamwe. Nadhani wanauza magari kwa passion na sio kutafuta pesa.

Ushauri: Kati ya kampuni zote hizo kwa kuangalia bajeti ya mtanzania wa kawaida, Real Motors is the best kwa sababu utapata gari nzuri na bei nzuri, hilo la customer care mtavumiliana.

Bajeti yangu mimi kwa FOB isizidi 6.5m najua hii kiasi napata IST kali tu
 
Back
Top Bottom