Naikumbuka Alexandria, Misri

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Montaza Palace, Alexandria June 1988


Ndugu zangu nilikuwa napita Maktaba Idara ya Picha.

Nia yangu ni kuandika kitu kidogo kuhusu mji wa Alexandria.
Katika pekua pekua nikakuta picha hiyo hapo juu niliyopiga Port Said Holiday Hotel.

Ilikuwa Jumatano Juni 15, 1988.

Hii picha yangu ikanishtua kidogo na kilichonishtusha ni mkao wangu. Nakuombeni muweke "caption," ya picha hii.

Alexandria ni katika miji mizuri duniani na sishi kuukumbuka lakini kwa sasa nitaukumbuka zaidi pamoja na magoli 5 waliyofungwa Simba na Al Ahly.

Ijumaa moja niliswali sala ya Ijumaa Montaza Palace, Alexandria. Hii ilikuwa kasri la Kiangazi la King Farouk na baada ya mapinduzi ya Gamal Abdel Nasser 1952 Montaza Palace ikawa moja ya majumba ya fahari ya serikali.

Ndani ya Montaza Palace kuna msikiti mzuri sana ambao niliswali Ijumaa nikifuatana na mwalimu wanvu mmoja kutoka Arab Maritime Transport Academy (AMTA) chuo kikubwa Arabuni yote katika mambo ya bahari.

Baada ya sala mwalimu wangu huyu akaniuliza kama nimeweza kuelewa khutba ambayo ilikuwa ya Kiarabu. Alishangaa nilipomwambia kuwa khutba ilikuwa kuhusu hijja. Nikamwambia nimeelewa khutba ile kutokana na aya za Qur'an kuhusu Hijja. Mwalimu wangu yule akaniuluza iweje nielewa Qur'an lakini sijui lugha ya Kiarabu?

Hii Montaza Palace ina sehemu muhimu moyoni kwangu kutokana kitabu cha Mohamed Hasnain Heykal, "The Road to Ramadan," alichoandika kuhusu Vita Vya Yom Kippur baina ya Misri, Syria na Israel mwaka wa 1973.

Baada ya mafanikio makubwa katika uwanja wa mapambano Anwar Sadat alikwenda Montaza Palace huku vita vikiendelea.

Heykal mwandishi mkubwa sana aliyekuwa mhariri wa gazeti la Alhram la Misri alikwenda Montaza Palace kufanya mahojiano na Sadat. Heykal katika staili yake ya uandishi wa "satire," kwa jambo asilopenda kwenye kitabu hicho anasema kamkuta Sadat ana glasi ya kinywaji.

Akampa swali.

Sadat hakujibu akaongeza kinywaji kwanza.

Taratibu akawa anakunywa hadi akamaliza ndipo akafungua kinywa chake akasema, "Mohamed mimi ni Amiri Jeshi Mkuu hayo maswali yako wapelekee wanasiasa Cairo watakujibu."

Katika sura hii Heykal anamnanga sana Sadat anasema uniform yake ya Commander in Chief aliagizisha kwa ‘’designer,’’ mabingwa wa mitindo ya nguo kampuni maarufu ya Paris - Yve Saint Laurent.

Kuna mengi ya kejeli Heykal kaandika...kila ninapoikumbuka Alexandria nakumbuka Montaza Palace, Sadat, Heykal...na goli 5.
 
 
Hatar sana hakika ulifaidi sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
salaam,
mzee wangu unamaanisha nini unapsema baada ya Sadaat kupata ushindi mkubwa kwenye uwanja wa vita? pia Misri iliwahi kutoa watu wawili watata sana ndg Ayman Zawahiri na bwana Sayyid Qutb bila shaka unawafahamu hawa
 
salaam,
mzee wangu unamaanisha nini unapsema baada ya Sadaat kupata ushindi mkubwa kwenye uwanja wa vita? pia Misri iliwahi kutoa watu wawili watata sana ndg Ayman Zawahiri na bwana Sayyid Qutb bila shaka unawafahamu hawa
Msaga Sumu,
Maana yangu ni kuwa vita vilikuwa vinawaendea vyema.

Hao ni maarufu ila kwangu mimi mtu mtata kutoka Misri ni
Osama Al Baz.
 
Msaga Sumu,
Maana yangu ni kuwa vita vilikuwa vinawaendea vyema.

Hao ni maarufu ila kwangu mimi mtu mtata kutoka Misri ni
Osama Al Baz.
s
Msaga Sumu,
Maana yangu ni kuwa vita vilikuwa vinawaendea vyema.

Hao ni maarufu ila kwangu mimi mtu mtata kutoka Misri ni
Osama Al Baz.
shukran sana,huyu Osama simjui ila acha nimtafute ni msome nae,hao wawili nilikutana nao kwenye kitabu fulani nikavutiwa nao sana
 
Mzee shikamoo, nashukuru kwa kutupa historia nzuri.
Samahani Ulipita katika chuo cha Arab Maritime Transport Academy (AMTA) kwa masuala ya kitaaluma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wangu tunaomba uandike vitabu ili utuachie zawadi ya kipaji na historia unayoifahamu.

Kupitia vitabu itakuwa ni zawadi kwa vizazi na vizazi pia mchango wako hautofutika kwa jamii yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee shikamoo, nashukuru kwa kutupa historia nzuri.
Samahani Ulipita katika chuo cha Arab Maritime Transport Academy (AMTA) kwa masuala ya kitaaluma.

Sent using Jamii Forums mobile app
Offshore...
Naam kulikuwa na program ya UNCTAD inaitwa Improved Port Perfomance (IPP) ilitengenezwa Chuo Kikuu Cha Cardiff, Wales ikawa inasomeshwa dunia nzima. Nilihudhuria mafunzo hayo na wanafunzi wengine kutoka Frontline States pamoja na Nigeria na Kenya na vyama vya ukombozi ANC, FRELIMO na wengineo. Walifadhili serikali ya Misri. Nitakuwekea picha In Shaa Allah.


Ismailia, Misri Juni 1988
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeandika vitabu kadhaa lakini maarufu ni kitabu cha Abdul Sykes kinachoeleza historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Mzee wangu tunaomba uandike vitabu ili utuachie zawadi ya kipaji na historia unayoifahamu.

Kupitia vitabu itakuwa ni zawadi kwa vizazi na vizazi pia mchango wako hautofutika kwa jamii yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran mzee, pia Epypt Air hutoa mar ubani wenye uzoefu wa kurusha ndege. Ukitaka kujua uzoefu wa rubani ni pale ndege inapotua husikii ile hali ya siafu kutembea tumboni mpaka kukukera.
 
Shukran mzee, pia Epypt Air hutoa mar ubani wenye uzoefu wa kurusha ndege. Ukitaka kujua uzoefu wa rubani ni pale ndege inapotua husikii ile hali ya disgust kutembea tumboni mpaka kukukera.
Sky...
Umezungumza kuhusu ndege - Egypt Air.
Nimepanda Egypt Air mara tatu.

Dar - Cairo - Dar.
Dar - Cairo - London - Dar
Dar - Cairo - Berlin - Dar
 
Gagnija,
Nimekuwa nikisafiri toka wakati Mkurugenzi Mkuu akiwa Peter Bakilana.

Hizo safari tatu nilizoweka hapo ya kwanza Dar - Cairo - Dar ilikuwa safari ya mafunzo Misri (1988).

Safari ya pili Dar - Cairo - London - Dar nilikuwa likizo (1991).

Safari ya tatu Dar - Cairo - Berlin - Dar nilialikwa Zentrum Moderner Orient (ZMO) Berlin kufanya mhadhara wa wazi na utafiti (2011).



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana mzee wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…