Naingia kwenye kufuga kuku chotara (Saso)

Mkuu, kuna kitu bado sijaelewa unamanisha nini hasa. Kwamba siyo vizuri kutotolesha mayai kwa kutumia kuku walio ya taga? If yes unadhani ni kwanini? Nahisi kuna point nzuri hapa ya kujifunza. Fafanua zaidi
kama hutojali.
 
Uzi wako mrefu Sana ola niliambiwa tu mayai yanayofaa kutotoleshea ni yale yaliyokaa sio zaidi ya siku 7 toka kutagwa. Hivyo ukizidisha mpaka siku 19 jua maya 30 yatakuwa jayana ubora hivyo hesabu yako hailipi
Nadhani hujasoma mpaka mwisho. Mayai yanaweza kukaa hata zaidi ya siku 30 Kama utakua unajua namna ya kuyahifadhi kwa kuzingatia joto stahiki na muelekeo wa mchongoko wa yai.

Na hesabu yangu inasema Kila baada ya siku kumi na sio kumi na Tisa.
 
Mkuu, kuna kitu bado sijaelewa unamanisha nini hasa. Kwamba siyo vizuri kutotolesha mayai kwa kutumia kuku walio ya taga? If yes unadhani ni kwanini? Nahisi kuna point nzuri hapa ya kujifunza. Fafanua zaidi
kama hutojali.
Huyu nadhani anaamisha uzao wa kuzaana kuku ndugu.

Wanashauri kuku wazaane angalau generation mbili tu. Baada ya hapo toa majogoo yote na utafute majogoo mengine ili kuondoa kizazi Cha kuku ndugu ambao Mara nyingi wanasumbuliwa Sana na magonjwa na wengi wanakufa wakiwa vifaranga.
 
Yes mkuu, hili nalifahamu. Nilishangaa hapo kwenye kuatamia mayai yao, nikahisi kuna shida katika hilo. Nimemuelewa sasa, alimanisha kuchukua mayai pengine kwa sababu za kuondoa hiyo issue ya "inbreeding".
 
Nzuri but kuku 25 wanakula debe 1 kwa mwezi?? Unawapunja!!
 
Nzuri but kuku 25 wanakula debe 1 kwa mwezi?? Unawapunja!!
Siwapunji, baada ya kuchanganya chakula Chao kwa fumula elekezi naongeza na majani(mchicha au chines) au hydroponic folder au azola na funza (wa kutengeneza mwenyewe kupitia pumba na mbolea ya kuku). Kwahiyo sio debe moja tu la pumba ni pamoja na hivyo vi gine
 
Safi mkuu..kikubwa andaa banda tu...
 
Uko vizuri. Nataka nijifunze hapo kwenye hydroponic folder na namna ya kutengenezs funza.
 
Uko vizuri. Nataka nijifunze hapo kwenye hydroponic folder na namna ya kutengenezs funza.
Kutengeneza funza ni rahisi

Chukua mbolea ya kuku iloweshe na maji weka kwenye ndoo au karai au chombo chochote chenye upana mzuri , chukua pumba za mahindi ziloweshe Kisha ziweke juu ya mbolea ya kuku iliyopo ndani ya chombo.

Then weka chombo chako eneo la wazi ili inzi waweze kufika kwa urahisi. Kila baada ya muda wa saa sita lowesha kwa maji na baada ya siku mbili mpaka nne utaanza kuona funza.
 
Uko vizuri. Nataka nijifunze hapo kwenye hydroponic folder na namna ya kutengenezs funza.
KUHUSU hydroponic ni shule ndefu kidogo jitahidi kutafuta Uzi humu unaelezea vizuri Sana kuhusu hiyo.

Jambo moja ambalo Uzi zote haujaeleza ni kwamba hydroponic folder kwa ajili ya kuku ni vizuri isizidi siku nne ili iweze kumeng'enywa kirahisi na kuleta matokeo chanya katika afya ya kuku.

Pia hydroponic kwa ajili ya kuku lazima ichukue nafasi isiyozidi 40% ya chakula chote cha Kila siku ili kuleta uzalishaji wenye tija kwa kuku wa mayai na nyama.
 
Nimefuga sasso 500 mwaka jana walikuwa wanakufa sana tofauti nanikifuga kroiler ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho.kila la kheri sasso mi mazuri kwa nyama siku kuhusu kutaga.sasso wanahitaji bio security yakutosha, hewa ya kutosha sio banda umetengeneza kama chumba cha kulala. Nasemea hao wengi maana 25 sio kaz kufuga.Dawa ya minyoo usisahau, Wape Newcastle wakifika minne.Ndui kama hawakuchanjwa watapukutika wote.muulize aliyekuuzia kama alichanja ndui.All the best
 
Njoo nikuelekeze jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku ila unatakiwa ulipie , njoo mp
 
Hongera mkuu kwa hatua, ila hapo kwenye ratio ya mitetea na majogoo naona haiko sawa mayai yanaweza kosa mbegu. Majogoo ni mengi sana kwa idadi ya mitetea yako. Majogoo hapa yangekuwa matatu tu.
 
Hongera mkuu kwa hatua, ila hapo kwenye ratio ya mitetea na majogoo naona haiko sawa mayai yanaweza kosa mbegu. Majogoo ni mengi sana kwa idadi ya mitetea yako. Majogoo hapa yangekuwa matatu tu.
Hili nitalizingatia. Majogoo yatayoonekana afya yake hainishawishi nitayafanya kitowewo
 
Hongera sana Mkuu
Naomba nikukumbuashe kitu kimoja Cha muhimu ambacho ujapanga kukifanya

✓Ipo ivi Jogoo mmoja anaweza kumiliki/kumudu matetea kumi ivyo inabidi uwe na majogoo mawili tuu

✓ kwa sababu majogoo ya saso Yana kucha Kali ivyo kama yakiwa mengi huwa yanapelekea vidonda kwa matetea hasa upande wa ubavuni na mgongoni hivyo inaweza kupelekea kifo au ulemavu wa kudumu kwaiyo majogoo mawili yanatosha Mkuu nakufanya kuku wako kutaga vizuri

Kila lakheri Mkuu
 
With thanks
 
Mimi pia nafuga ninao Saso 100 now
Naweza sema wanahutaji full time care
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…