Naingia kwenye kufuga kuku chotara (Saso)

Niliwanunua wakiwa wameshapata chanjo zote. Kwa Sasa ni marudio tu ya chanjo ya kideri.

Kuhusu dawa nilipata changamoto ya mafua nikawapa mchanganyiko wa tangawizi, vitunguu swaumu na pilipili. Wakakaa sawa. Baada ya muda ikajirudia Tena nikaamua kutengeza mazingira wawe wanalala juu ya wavu. Huenda nikapunguza maradhi kwa % kadhaa
Vp kuhusu chanjo na madawa ya kuku?..halafu kuhusu chakula hiyo debe moja na nusu ni makadirio ya chini mno. Mimi binafs ni mfugaji wa kuku.

 
Mkuu hongera kwa uthubutu na kila la kheri katika ufugaji, mrejesho wako kwa kila hatua utakua mchango mzuri kwetu.

Mimi na bro tuliwahi kujaribu kuwafuga 12 tu kama majaribio ilienda poa mayai tuliyala kiasi na wawili wa mwisho walikua wakubwa kiasi kwamba kwenda kumchinja unaogopa atakugeukia[emoji16]...
 
Ndugu yangu samahani naomba unisaidie namba yakoo nahitaji nikuulize kitu kuhusu hii kitu uliyoandika hapa. Ubarikiwe🙏.
 
Hili nitalizingatia. Majogoo yatayoonekana afya yake hainishawishi nitayafanya kitowewo
[emoji23][emoji23][emoji23]acha kuyafanya kitoweo mkuu bora ubadilishane na mtu anayeuza kuliko kula sababu kila dhaifu utakua unakula

Ni mawazo yangu tu
 
ufugaji wa kuku naupenda ila shida ilikuw inakuja siku ya jmoc na jpili nikimaliza kuwafanyia usafi na kuwapa chakula akili inaniambia chomoa mmoja ujipongeze.

nikaona isiwe tabu nikaweka mfanyakaz hapo ndo nikaharibu mradi kabsaaaa,dogo anaenda kuuza kuku anapata hela yuleee kwa mademu badae analeta story mara kuku amekufa nimemtupa.

safari hii nimendaa 1m naingia mazima sitaki masiara tena.
 
Hongera Sana kingkongtz Nami ntakutengenezea sehemu ya kuzalisha hydroponic fodder. Zinapungiza mno gharama ya ulishaji. Kuku (na ndege wengine) na wanyama kama mbuzi, ng'ombe, nguruwe, sungura wanafurahia kula chakula hiki.
 
[emoji120]
 
Asante Sana.
 
MREJESHO BAADA YA MIEZI MITATU.

Leo tarehe 1 April ni miezi mitatu imepita tangu nimeanza mradi huu. Na huu ni mrejesho kwa vijana wenzangu ili watakapoanza wajue muongozo sahihi.

Nilifanikiwa kununua kuku wengine wakafika jumla 60. Lakini wakapungua
Mpaka Sasa wamebaki 50. Mpaka Sasa nimezika kuku watano wawili kwa ajili ya ugonjwa na watatu walikua wadhaifu wameuliwa na majogoo wakati wanawapanda Mara kwa Mara.

Kuachana na vifo mradi unaenda vizuri, japo mafua na kuharisha ilikua ndio changamoto kubwa lakini kwa Sasa nimeweza kuidhibiti.

Kuku wamekua wakubwa, Ila changamoto hawana uwiano sawa wa ukuaji, hii ni kutokana na wakati nna wanunua walikua hawana ukubwa sawa japo walikua Wana umri sawa.

Mpaka Sasa hawajaanza kutaga japo wanatetea Sana. Nimeambiwa changamoto inaweza ikawa lishe ya awali(yaani wakati wakiwa vifaranga au lishe ya Sasa). Yaani wanasema kuku anaetakiwa kutaga baadae analishwa tofauti na kuku anaetakiwa nyama kipindi Cha kifaranga(bado nafanya utafiti nitaleta mrejesho)

Lakini pia wanasema kuku ukimlisha chakula chenye mashudu mengi, mwili unatengeza mafuta Sana na kuharibu mfumo wa mayai(bado nafanya utafiti nitaleta mrejesho)

Nimefanikiwa kuuza kuku mmoja kwa sh 18,000 na nimepanga kupunguza majogoo kwa sh 20,000 pasaka hii. Na Kama utafiti juu ya chakula kipindi Cha kifaranga kinaweza kuwa sababu ya kushindwa kutaga vizuri au kutaga kabisa basi nitawauza wote nianze upya

Nimefanikiwa pia kutengeneza mashine ya kutotolesha mayai (incubator) ambayo Jana tarehe 31 March imefanikiwa kutotolesha mayai 42 Kati ya 53 ya kanga na mayai 60 Kati ya 60 ya kuku.
Mashine hii Ina uwezo wa kutotolesha mayai tray 6 sawa na mayai 180 mpaka 200.

Mpango ni kutengeneza nyingine ya mayai 720 mapema mwezi huu baada ya kupata matokeo mazuri ya mashine ya awali.

Nitaendelea kutoa mrejesho kwa maendeleo zaidi. Asante
 
Unatengeneza incubator mwenyewe?
 
Hongera chief.....ila nikwambie kitu, hutapata mayai zaidi ya matano kwa siku.

Sasso sio a layering breed....ni kuku kwaajili ya nyama. Uwezo wao wa utagaji ni mdogo sana, na ni chini ya asilimia 30 kwa siku.

Tafuta breed nzuri kwaajili ya mayai. Nakuhakikishia hutapata mayai zaidi ya matano kwa siku. Nitafute kwa mwongozo zaidi.
 
Hivi hakuna crossbreed ya kuku wa kienyeji na wa mayai, ambao wanatoa mayai kedekede?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…