Naingia kwenye kufuga kuku chotara (Saso)

Hongera Mkuu kwa kupiga hatua, hawa Kuku namna unavyowapa chakula kinachangia katika kuwafanya wawe wanataga kwa sana Mayai au wa Nyama...

Kipindi tunanunua Mzee aliyetuuzia alituonyesha kuku ambao aliwalisha vizuri kwa ajili ya nyama wanavyokua, na wale aliowalisha kwaajili ya mayai wanavyokua. Pia akatupa na formula ya chakula kuanzia wakiwa wadogo mpaka wanakua kwaajili ya kutaga mayai sema sasa karatasi nililoandikia hzo formula sikumbuki niliweka wapi ila ukipata wataalamu wanaweza kukusaidia.
 
Fanya tafiti kijana. Usilazimishe matokeo ulioyapata kwako iwe ndio final say.

Kwa Sasa nimeanza kutotolesha wa Malawi. So nitakuwa na breed mbili na nitaleta mrejesho
 
Nimefuga hawa kuku na wife ndio msimamizi mkuu ila tumekosa wateja.
Idadi 150 wapo kahama wana miezi 5. Tufahamishane kwa anaejua wateja maana nimeweka tangazo humu na kuzunguka kahama lakini hola
Unawauza Bei gani na wamefikisha uzito kiasi gani? Pasaka inakuja endelea kufanya matangazo huenda Mambo yakawa mazuri.
 
Fanya tafiti kijana. Usilazimishe matokeo ulioyapata kwako iwe ndio final say.

Kwa Sasa nimeanza kutotolesha wa Malawi. So nitakuwa na breed mbili na nitaleta mrejesho
Hongera Mkuu
Upo mkoa gani
 
Upo sahihi Mkuu lkn kuku wa sasso ni chotara ivyo anaweza kufungwa kwa ajili ya nyama au mayai so chakula ndio kinacho fanya awe wa mayai au wa nyama na sio Breed kama unavyo zani ww

Ipo ivi endapo utampa 18-20 % ya protein kwenye chakula pindi akiwa na umli wa 1-8 week then ukampatia 16-18% ya protein pindi akiwa na umli wa 9-16 then kwanzia week ya 17 na kuendelea ukimpa 18-20 ya protein basi utagaji utakuwa juu lkn endapo protein ikawa juu Zaid ya apo wazi kutaga

Pia kuku aina ya sasso anavyo kuwa na umli wa 16 na kuendelea inabid apate mwanga kwa masaa 16 pia Giza kwa masaa 8 kwasababu atafanya utakagaji utakuwa mkubwa maana pituitary grand ya kuku inakwa active endapo ikipokea mwanga kwa masaa 16 ivyo kufanya kazalisha homorne ya utengenezaji wa mayai kwa kiasi kikubwa
 
Natunza hii kwa matumizi ya baadae.
 
""Baada ya mvua za msimu huu kuwa za kusita na kupoteza mbegu kwa kupanda zaidi ya Mara mbili na kuungua na jua""

Hii πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘† ni nini?
Mpunga au?

Ila pia kuku ratio huwa ni matetea 10 - 12 kwa jogoo mmoja.

#YNWA
 
Namba mbili naomba unifunze vizuri mkuu
 
Ilikua nyanya mkuu Ila nashukuru nilifanikiwa kuvuna na Sasa naweka Tena mbegu chini kwa ajili ya msimu wa April mpaka kiangazi.
""Baada ya mvua za msimu huu kuwa za kusita na kupoteza mbegu kwa kupanda zaidi ya Mara mbili na kuungua na jua""

Hii πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘† ni nini?
Mpunga au?

Ila pia kuku ratio huwa ni matetea 10 - 12 kwa jogoo mmoja.

#YNWA
 
Namba mbili naomba unifunze vizuri mkuu
Anamaanisha uwajengee Banda ambalo watakaa juu kwenye wavu ili mavi yawe yanadondoka chini.

Nitashare picha uone inavyokua
 
Nimefuga hawa kuku na wife ndio msimamizi mkuu ila tumekosa wateja.
Idadi 150 wapo kahama wana miezi 5. Tufahamishane kwa anaejua wateja maana nimeweka tangazo humu na kuzunguka kahama lakini hola
Hao unaweza kuwauza kwa kiwanda Cha alpha choice wananunua kuku kwa ajili ya kuwaprocess kuwapeleka nchi za uarabuni ni pm nikuunganishe na fomeni wa kiwanda UWE unauza kwao wananunua kuanzia kuku 50 na kuendelea

sent from HUAWEI
 
Shukrani mkuu
 
Mimi nniliwafuga saso na walitaga kila siku. Niliwapa chakula kidogo Cha kuchanganya na makombo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…