Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Wanaukumbi
Baada ya Uchaguzi wa ndani wa CHADEMA kuisha na kupata viongozi wa wapya Mwenyekiti Tundu Lissu, na Makamu wake John Heche.
Kama tulivyosikia na kuona hotuba ya Mwenyekiti aliyepita Freeman Mbowe, kuwa uchaguzi umeacha mpasuko mkubwa ndani ya chama ingawa hawa viongozi wapya wanajifanya kama hamna kitu kilichotokea, ukimuangalia Mbowe alivyokuwa anaongea unaona wazi kabisa kaondoka CHADEMA na kinyongo moyoni na usaliti aliyofanyiwa na baadhi ya wenzake ambao alikuwa anaona ni watu wake wa karibu kumbe maadui zake
Hawa wasaliti walimchafua sana Mbowe, kwenye mitandao ya kijamii kumtukana kwenye mitandao kumuita mla rushwa mkubwa hana uchungu na CHADEMA, msaliti mkubwa alikuwa Lema, na wenzake amba walitumwa na kumshambulia Mbowe, leo hii wamesahu mchango wa Mbowe katika Chadema Lema, kamsaliti Mbowe, watu wa Kaskazini ambayo ilikuwa ngome ya Chadema. Wamasikitishwa sana na wengi wapo kimya wanasema adhabu yao wataitoa October.
Soma Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%
Hamna kipindi watu wa Kaskazini wameumizwa kama hiki kipindi kiongozi wao mkuu Mbowe kushambuliwa, kutukanwa kudhalilishwa na kina Lema, na genge lake, baada ya Uchaguzi hawa viogozi wanaanza kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kuanza kumsifia kinafiki nani alikuwa anajua kama mkutano wa Chadema maandalizi yote pesa katoa Mbowe zaidi ya Milioni 300. Lema na wenzake walisema hili.
Nimeongea na watu wa Kaskazini wengi wanasema bora waende wakatulie kwa Mama tu CCM.
Kimsingi Lema na Lissu. Siyo wakazi wa Tanzania, Lema famila yake ipo Canada na Lissu familia yake wapo Marekani na Ubeligiji. Wote wanatembea na tiketi mfukoni.