Naiona Simba ikifika nusu/ fainali Kombe la Shirikisho Afrika

Naiona Simba ikifika nusu/ fainali Kombe la Shirikisho Afrika

Mr. Sound

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
2,227
Reaction score
4,773
Wakuu salaam,

Simba chini ya Pablo imekua na mabadiliko ya haraka sana, ukiwatizama wachezaji unaona kabisa ile nguvu, ari na uchu wa kuipambania team vimerejea kwa kishindo.

Ukiyatizama mashindano ya shirikisho kwa ujumla, utaona team kubwa shindani kwa simba ni TP MAZEMBE & PIRAMYD, kwa niionavyo Simba chini ya pablo uwezekano wa kufika nusu/final ni mkubwa sana na kama mungu atapenda pengine tunaweza kabisa kuibeba ndoo ya shirikisho.

MUNGU IBARIKI SIMBA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Shida kubwa ya wachezaji wa Simba ni dharau na kurelax kama sio dharau hata msimu uliopita CAFCL wangefika nusu na hata final pia.
Hata mechi na Jwaneng pia kurelax kuliwaponza.
kwa sasa wamejifunza, sidhani kama watamchukulia poa mpinzani yeyote
 
Unajua Kama Tp Mazembe, Orlando Pirates Rs Berkane Wapo Pia Au Unaongea Ongea Tu Kwakuwa Juzi Mmewafunga Vilema
 
Wakuu salaam,

Simba chini ya Pablo imekua na mabadiliko ya haraka sana, ukiwatizama wachezaji unaona kabisa ile nguvu, ari na uchu wa kuipambania team vimerejea kwa kishindo...
Ungesema unatamani kuiona simba inavuka robo fainal, vinginevyo kama ukimwuliza shaaiki yeyote wa simba kuhusu hatua anayodhan simba itafika, atakuambia simba wanachukua ubingwa africa.
 
Unajua Kama Tp Mazembe, Orlando Pirates Rs Berkane Wapo Pia Au Unaongea Ongea Tu Kwakuwa Juzi Mmewafunga Vilema
mbona Tp nimewataja kwenye bandiko, hizo team nyingine ni za kawaida.
 
Bado kuna timu zenye ubora sana huko group stage.

Simba inabidi waendelee kukaza,nimependa mada CEO anavyowapa malengo.

Lazima wapambane sana.
 
Back
Top Bottom