Yanga lazima wafuzu.
Wasipofuzu mgogoro mkubwa sana utaibuka.. kwa navyojua nguvu ya wanachama na mashabiki wa yanga sitashangaa hata aziz ki akaambiwa asepe
Engineer hersi na wachezaji wa yanga + benchi la ufundi hawawezi kubali hilo litokee hivyo ni lazima wafuzu kwa mbinu yoyote hata kununua mechi kwa hela nyingi sana
Kwamba matokeo yatakuwa yanasubiri yatoe favour kwa Yanga kwasababu ya kuepusha conflicts za viongozi?
Mashabiki wanaodhani viongozi wamepelekea Yanga kupata matokeo haya watakuwa ni mashabiki wajinga
Kwa hoyo kwasababu wao ni unbeaten walitaka wawe hivyo hivyo kila siku na kwamba siku ikitokea wamepoteza basi moja kwa moja sababu iwe ni viongozi?
Akili za namna gani hizi?
Mayele anakosa mabao, kakosa magoli ya wazi si chini ya mawili
Uongozi unahusika vipi na swala hilo?
Na Mayele swala la kukosa magoli sio jambo geni, maana mechi tatu za mwisho alizocheza alikuwa anakosa magoli.
Na wapo mashabiki ambao walikuwa wanavimba kuwa "hicho ni kipindi cha kwanza na huo ndio mfumo wake ila kipindi cha pili lazima atupie"
Lakini leo sasa wameanza kuona umuhimu wa zile nafasi alizokuwa anakosa kwasbabu wanasema huwezi kujua thamani ya kitu mpaka pale utapokipoteza
Thamani ya zile nafasi alizokuwa anakosa kwenye mechi na Zalan zilikuwa covered na ushindi hazikuweza kujadiliwa kuwa ni mistakes na pengine hao hao mashabiki wangemsikia mtu anazungumzia jambo hilo wangemuita hater.